JE ULIWAHI KUISHI KWENYE MAHUSIANO/NDOA NA MTU AMBAYE AMEKUFANYA KAMA DARAJA LA MAFANIKIO YAKE🤷🏽‍♂ - EDUSPORTSTZ

Latest

JE ULIWAHI KUISHI KWENYE MAHUSIANO/NDOA NA MTU AMBAYE AMEKUFANYA KAMA DARAJA LA MAFANIKIO YAKE🤷🏽‍♂

Unhappy Young Woman Having Argument With Man At Home Stock Photo - 55432731
Bin adam tuna tabia tofauti iwe kwa maumbile ama hulka za ki malezi, Upendo mwingi hugeuka kuwa teso kwa yule anayejitoa MWILI, AKILI NA MOYO WAKE kwa ajili ya kumpenda mtu... Sisemi TUSIPENDANE laa hasha🤦🏾‍♂ ni tendo linaloashiria UBIN ADAM japo hata viumbe wengine wanapendana Kwani hujawahi kuwaona kumbikumbi🦗? Wapo watu hutamka NAKUPENDA kama ishara ya pumbazo kwa mwenza wake, Mtu anaweza kulia ama kujiuguza ukadhani MPENZI SI HUYU SASA lakini ni mhunzi wa MAPENZI FAKE🙆🏿‍♂
Kikubwa alichonacho pengine aliishajua NYOTA YAKO inapandisha maisha yake, Wakati unakutana nae hata muonekano hakuwa nao ila leo kila mtu anapomtazama anam-admare 👌 swali je anakumbuka alikotoka? Wengi wenye tabia hizo hujihesabia haki kwani wamejawa ubinafsi, Mtu anapokufanya DARAJA la mafanikio yake kamwe hatajwi kwa upendo bali ni kwa masrahi yake, Watu hao kila ukitaka kumuacha TARAJIA KUONA PIPA LA MACHOZI😭
Lakini ukimpa kisogo tu ANAKUNG'ONG'A🤣 mtu huyo ni hatari kwa maisha yako Kwani iko siku ambayo haina jina ATAKUMWAGA HUTAAMINI Kwani anaweza kukuvumilia kwa sababu malengo yake hayajatimia ngoja atimize malengo yake utaita Mama na alishatangulia mbele za haki😎
Machozi hayatoki moyoni, Kilio cha kwikwii na huzuni nyingi hazitoki moyoni, MOYO wa mtu ni ficho la kile anachokipanga sasa wewe endelea kumuonea huruma mwenzio kwa masrahi yake aje atusue akumwage🍻 ujutie kumvumilia wakati huo mwenzio atakuwa ANAIPEPERUSHA BENDERA🚩 ya penzi jipya na mtu ambaye hata hakumuombea kwa MUNGU kwa mafanikio aliyopata huku wewe ukiachwa UNAPAUKA TU😏 kataa kuwa DARAJA LA MAFANIKIO Ya Mtu laa kama unaamini safari yenu ni moja, Muda ni mali isiyooza ila inapitwa na wakati, Sasa wewe endelea kubembelezwa ukidhani unapendwa kumbe mwenzio anatembelea NYOTA YAKO 🎇
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🕺




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz