Chukua hii itakusaidia 😘 - EDUSPORTSTZ

Latest

Chukua hii itakusaidia 😘

Image result for mapenzi wakubwa
Ukiona kuwa kila ukitongozwa na mwanaume unaenda kumuambia Rafiki yako basi jua kuwa wewe ushavunja ungo lakini akili zako bado hazijavunja ungo. Tena kuna wale anatongozwa anaanza kumuonyesha shoga yake meseji na wanazijibu pamoja mnacheka, majifanya mnamchora mwanaume kumbe ni utoto , badilika jifunze kukataa mwenyewe.
(1) Kama hujaolewa basi jua kuwa kuna uwezekano mkubwa huyo huyo rafiki yako uneyemuambia mambo yako akakuharibia! Hivi hujiulizi, yeye mwenyewe hana mahusiano, au ana kile kijamaa chake kinamsumbua balaa, halafu unamuambia kuwa wewe unatongozwa na flani sijui ana hela sijui hivi na vile kana kwamba hamtaki! Aisee labda kama mwanaume mwenyewe halipi, kama analipa atakuharibia na kujitongozesha yeye na kama halipi basi atakuharibia tu ili mkose wote mbaki na visirani, apate mtu wa kumsindikiza kwenye kisirani chake.
(2) Kama umeolea basi jua kuwa huyo rafiki yako mkizinguana kila kitu anaenda kumwagia mume wako, yaani hataishia kusema tu flani alikua anamtongoza basi atasema mlitembea naye.
Ushakua mtu mzima, kama unatongozwa hutaki kataa, mambo ya kuuliza uliza sijui kuonyeshana DM eti na mimi kanitongoza ni ushamba na utoto wa kizamani! Wengine wanawaza sasa nitajuaje tabia za huyu mwanaume kama sitauliza watu, aisee hata ukiuliza hutajua, lakini kuna uwezekanao ukapata uongo ila kama unataka ukweli usiulize kama vile unamtaka au mwanaume kakutongoza bali uliza kama vile unamjua au unataka tu kumjua basi.
Kwa mfano “Hivi huyu Kaka yuko TRA… huyu Kaka si ndiyo yule hivi na vile, huyu Kaka mboga sana, sama naona hivi na vile…” chunguza kama unataka kumjua na si kama mwanaume anakutaka. Wanawake wanaona wivu sana marafiki zao wakiwa au wakitakwa na wanauem wanaojielewa!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz