Binadam anazo safari nyingi awapo DUNIANI lakini iko safari moja ngumu ambayo hiyo ndiyo IMEWAANGAMIZA wengi; - EDUSPORTSTZ

Latest

Binadam anazo safari nyingi awapo DUNIANI lakini iko safari moja ngumu ambayo hiyo ndiyo IMEWAANGAMIZA wengi;

Image may contain: one or more people
SAFARI YA MAHUSIANO/NDOA
Kwa hakika hii ndiyo safari ambayo haina MSOMI, TAJIRI, MWANA MASUMBWI aliyeingia ndani ya safari hii akatoka kama alivyoingia, kuna walioingia weupe wakatoka weusi, kuna walioingia wanene wakatoka wamekondeana, kuna walioingia WANA MALI lakini wakati wa kutoka walikuwa masikini, Safari ya MAHUSIANO/NDOA Mtu anaingia akiwa mwenye FURAHA akiwa na hakika kwamba AMEMPATA AMBAYE ATAJUA KUITULIZA NAFSI YAKE.
Lakini safari inapoendelea ndivyo MAFANIKIO yanakuja ama kutoweka, Lakini ukiishaingia na kukuta SALAMA unamshukuru MUNGU ila kama ndo ukakutana na ndivyo sivyo basi wengi wamebakia kugugumia MAUMIVU na wala wasijue namna ya kujinasua.
Inauma sana kuwekeza;
MOYO
AKILI
MWILI
Kwa mtu ambaye hakuwahi kufikiria kuwa na wewe, Kwa sasa watu wengi ni WAHANGA WA MAPENZI iwe kwa uhusiano ama ndoa lakini maana halisi ni MAPENZI.
Kutokana na uhanga wa MAPENZI wengi wanajikitika katika kutafuta RELIEF ya mioyo yao na sio kutafuta hakika ya UPENDO
Unakuta Mtu anajinasibu KUMPENDA mwingine wakati hajamaliza tatizo linalomsababisha kutafuta Mtu mwingine, Yaani kabla hajajua hatma ya tatizo alilopo tayari anadandia uhusiano mwingine ili kupoza STRESS
Na hilo ndilo JANGA LA KIMATAIFA Kwani DUNIA nzima inaomboleza Swala la MAPENZI
Mtume PAULO hakuwa mjinga kusema;
"MNGELIKUWA KAMA YEYE WALA MSINGESUMBUKA NA HIZI VITU VYA KWICHIKWICHIII"
Maana alijua hiyo radha imewekwa mahala pabaya sana, kwamba ni mamlaka ya mtu KUKUPATIA AU KUKUNYIMA
Bora utamu huo ungewekwa kwenye TEMBELE Yaani linaota popote na ukitaka kula wala hakuna gharama, Lakini akawekewa MANKA/JUMA wallah ni mateso mpaka kufa😅😅
Safari ya MAPENZI Mtu ukiianza HUFIKI na ukitaka kushuka UNAPEWA MATUMAINI mwisho huuoni, Kufika ni ndoto, Basi inakuwa ni AFADHALI YA JANA😭😭
Kuliko kusafiri safari moja na watu wawili BORA UWE NA MMOJA KWA HITAJI LA NAFSI YAKO iwe kwa ugumu ama wepesi kikubwa UMERIDHIA MWENYEWE KUWA NAE
Kuwabeba watu wawili kwa wakati mmoja iko shida wengi hamuijui nayo ni;
"KUONEKANA UNAPENDA NGONO"
Kwa sababu Mmoja hakutoshelezi lakini kumuacha hutaki, Maana yake wewe ni MBINAFSI😂
Fikiria pia KUJIHESHIMU MWENYEWE KABLA HUJAHESHIMIWA Kwani heshima inatokana na MATENDO yako.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨🔨🔨
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz