AMUA KUISHI LEO, ACHANA NA YA JANA! - EDUSPORTSTZ

Latest

AMUA KUISHI LEO, ACHANA NA YA JANA!


Uliumbwa siku moja, uliingia tumboni mwa mama yako siku moja, utakufa siku moja! Hivyo amua kuishi kwa siku. Usibebe ya jana na kwenda nayo kesho yake maana jana ilishapita.
- Hivyo kama ni mpambano, pambana leo umalizane nao leo.
Maelekezo ya leo sio ya jana wala ya kesho, hivyo fuata maelekezo ya leo kwa bidii maana kesho yatakuja mengine.
- Siku shetani akiinuka kinyume chako usiseme utamalizana nae kesho, bali malizana nae leoleo. (usiweke viporo) Mungu akiona umedhamiria leo yako itokee leo, anakutia nguvu ili uikamilishe.
NEEMA kazi yake ni kukubeba kutoka pale uliposhindwa ili uweze kushinda. Ila kwanza AMUA leo yako iwe LEO.
AMUA KUISHI KATIKA SIKU.
- Kama unataka kuwa BORA, ishi kwa SIKU na umaskini hautakung’ang’ania.
© I DO LOVE EFATHA
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz