VIASHIRIA 6, MWANAMUME MWENYE UWEZEKANO MKUBWA KUKUSALITI UNAPOKUA NAE KWENYE MAHUSIANO. - EDUSPORTSTZ

Latest

VIASHIRIA 6, MWANAMUME MWENYE UWEZEKANO MKUBWA KUKUSALITI UNAPOKUA NAE KWENYE MAHUSIANO.


Kasi ya usalit inaongezeka siku HADI siku, mwanamke anaweza kujiuliza swali hili,kama nimeweza kuchepuka na mume wa mtu na akatamani kuitelekeza familia yake kwa ajili yangu, je nikiolewa itakuwaje?? Mume Si ataweza kunisaliti kwa wanawake wengine?
Hapa nmekuwekea viashiria vinavyoweza kukusaidia kujua mwanamume uliyenaye au utakaye kua nae anawezakukusaliti muda wowote bila wewe kujua au kwa kujua.
1. Mwanamume anayependa tendo la ndoa mara kwa mara zaid kuliko mke wake anavyopenda.
Kama mwanaume anapenda ngono kiasi kikubwa kuliko mwanamke , hasa yule aliyewahi kua na Wapenzi wengi kwa wakati mmoja hatotosheka,tegemea tu atakusalit na wengne.
2. Mwanamume anayependa kutoka au kusafiri mara kwa mara, tegemea atachepuka.
3. Mwanamume anayependa kua na marafik wengi wa kike
Kuna wanawake hujisifia kua na marafik wa kiume, tafiti znaonesha kwa mwanamke inawezekana kuishi na mwanaume na kumfanya rafiki lkn kwa mwanaume haiwezekani, mwanaume ameumbwa kwa matamanio Kwahyo atatamani tu, na hisia zikishajengeka hapa, mwanamume ni rahisi kuchepuka.
4. Mwanamume mwenye marafik wazinzi, ataiga tabia za wenzie, wanaume walioacha familia zao , wasio kwenye mahusiano na mtu mmoja.
5. Mwanamume ambaye alishawahi kusalitiwa, huyu ipo siku anaweza kukusalit maana kwenye akili yake tayari kuna jinamizi limekaa limemwaminisha wanawake sio wa kuaminika, sio waaminifu, hivyo ataishi na wewe lkn naye hatokua mwaminifu kwa Mentality hii. Mwanamume msaliti aliyewahi kusalit nyuma na hajakamatwa pia anauwezekano wa kuendelea kua msalit hasa pale atakapo kutana na utamu mpyaa.
6. Mwanaume aliyewahi kua na wapenzi zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. Huyu pia ni rahisi kuwa msaliti. Na kuendelea na tabia hiyo.
Jifunze kumfahamu vizuri mtu uliyemchagua na mazito au mepesi aliyoyapitia au aliyoyafanya kabla yako, yatakusaidia namna ya kumpenda na Kufanya uchaguzi usio kua na majuto baadae.
J4REAL-TECK
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz