UNAISHI KWENYE NDOA LAKINI BADO UPO SINGLE BILA KUTAMBUA: - EDUSPORTSTZ

Latest

UNAISHI KWENYE NDOA LAKINI BADO UPO SINGLE BILA KUTAMBUA:


Mm naamin maana halisi ya kuwa single ni mtu kuwa pekeyako, kujimiliki, kujihudumia mwenyewe na kufanya mambo yake binafsi binasfi. Hata vile ambavyo anaishi ni maisha yake ya usingle ameyachagua yan haambiwi na kitu wala hapelekeshwi na mtu yeyote.
πŸ‘‰Hizi ndio ndoa za sasa zilivyo, wanandoa wanaishi kama wapo single bila kujitambua. Ndoa zimekuwa hazina maelewano, isitoshe kila mtu anafanya mambo yake anavyojua kwa wakati wake na kwa utaratibu wake yan hakuna muunganiko wowote ambao unaeka alama ya wanandoa.
πŸ‘‰Baba anaenda kivyake, mama anaenda kivyake, Wakati mwingine hata mawasiliano hakuna baina ya mume na mke, Lakin utashangaa kuona mwenzio yupo bize na sim na wala hashughuliki na ww, hakutafuti. Hakuna mtu wa kujali hisia za mwenzie kati yenu, kila mtu anaishi kama yupo single.
πŸ‘‰Ndani ya nyumba mnaishi wawili nyie ni wanandoa mliooana, lakin baba ananunua vitu vyake mwenyew, mama nae ananunua vitu vyake mwenyew, Kila mmoja anajimilikisha vitu vyake mwenyew hakuna kielelezo cha kwamba nyie ni wamoja, Bado inaonekana mpo single lakin mmejificha kweny kivuli cha ndoa.
πŸ‘‰Unakua bize kiasi kwamba unashindwa kuongea na mwenzio, huwez kukaa chini na mkeo/mmeo mkazungumza mambo ya kifamilia, mwenzio akikuongelesha unamuona mwehu, saa zote upo bize na simu yako, upo bize na shoga zako, upo bize na tv yan upo kama upo mwenyew upo bize na mambo yako mwenyew mwenyew.
πŸ‘‰Kwann unaishi na mwenzio kwa kivuli cha ndoa, ilhali na ww uonekane ni mwana ndoa. Unakaa na mwenzio bila malengo bila muunganiko wa kiuhalisia kwamba ninyi ni wanandoa. Unaishi maisha yako ambayo hutaki kuulizwa kwann hivi au kwann unafanya hvyo.
πŸ‘‰Kitu ambacho kinapelekea usingle katika ndoa zetu ni ujuaji baina ya wanandoa, dharau, kudharauliana, kutokusikilizana kila mtu ana sauti juu ya mwenzie, baba akiwasha moto mama nae anawasha. Kwahyo unakuta hakuna maelewano na kunaingia kiburi ndani ya wanandoa kila MTU anafanya mambo yake, hapo ndipo upweke na usingle unapoanzia.
πŸ‘‰Ebu itafakari ndoa yako wew mwanamke na mwanaume jee kwa namna unavyoishi unaona unaishi ndani ya ndoa au unaona uko pekeyako. Maana kama kila jambo unalifanya pekeyako bila tamko na wawil kama wanandoa ni dhairi shairi unaishi single. Jitafakari fanya maamuzi ndoa ni mwili mmoja, kunia mamoja na kushirikiana kwa pamoja.
J4REAL
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz