Ukisalitiwa kwenye mapenzi una haki ya kuumia na hakikisha unalia kwa uchungu wako wote ili usije kulia tena kwa kosa la kusalitiwa.
Mungu hukupa mwenza wa kukufariji na sio kukusaliti, ndio maana ukiumizwa kwenye mapenzi Mwenyezi Mungu hukuonyesha aliyekuumiza kuwa hakufai.
Aliyekusaliti huomba second chance, akiwa na maana risasi ya kwanza hakuitumia vyema ndio maana anaomba nafasi ya pili.
Ukiona Ex wako aliyekuumiza anarejea kwako jua Malaika wanataka kujua kama wewe bado ni mpumbavu kwa Mara ya pili au umeshajifunza kutokana na makosa,mtu anayekupenda hawezi kukuumiza.
Ukimsamehe mpenzi aliyekuumiza hakikisha unamuamini ila ukimsamehe na kutomuamini ni bora kutokuwa naye ukabaki mwenyewe.
Wanaopenda kusoma mambo ya mapenzi ni wale walioumizwa kwenye mapenzi na waliopo kwenye mapenzi bora hupenda kusoma mambo ya msingi sababu teyari wana mapenzi ya dhati.
@J4REAL-TECK
No comments:
Post a Comment