#NINGEJUA ni hali halisi ya maisha ya wanandoa wengi - EDUSPORTSTZ

Latest

#NINGEJUA ni hali halisi ya maisha ya wanandoa wengi

Image result for UTAMU WA PENZI


"#NINGEJUA......”
✍️ Ndoto na matumaini ya kila mmoja wetu wakati tulipoufunga ndoa, yalikuwa kuishi maisha yaliyojaa upendo, furaha na amani tele. Na ndizo ndoto za wengi wanaofunga ndoa.
✍️ Kwamba, maisha yao yawe ya furaha. Lakini mambo yako kinyume kabisa na matarajio hayo. Utafiti ulliopelekea kuwepo Kwa Neno #NINGEJUA umeleta matokeo ya kusikitisha sana ambapo watu 170 kati ya 200 wanajuta kufunga ndoa na wenzi wao na kama wangejua tabia zao zitakuwa walizonazo sasa, wasingekubali hata kwa bakoraKadhalika, wanandoa 122 kati ya 200 wanakiri kufunga ndoa na watu ambao hawakuwapenda kwa dhati na hawakuwa chaguo lao
✍️“Kama ningejua Mume wangu atanitendea haya, nisingekubali kuolewa hata kama ingebidi kufa” “Kama leo Kanisa litatoa ruhusa ya kuachana, mimi nitakuwa wa kwanza kumpa Mke wangu talaka”. Majibu haya yanadhihirisha kuwa Wanaume na Wanawake wengi wamezichoka ndoa zao kwa namna isiyotarajiwa.
✍️ Hawana hamu na wenzi wao na wangependa hata pengine, Mwenyezi Mungu afanye miujiza itakayosaidia kuachana nao haijalishi ikiwa ni kwa njia ya kifo Ndoa zimetawaliwa na vilio na majuto kama ilivyodhihirika wakati wa utafiti uliopelekea kuandikwa kwa neno #NINGELIJUA
1. KAMA UNGEJUA MUMEO ATAKUWA NA TABIA ALIYONAYO SASA UNGEKUBALI
AKUOE (a) Ningekubali (b) Nisingekubali
✍️Katika swali hili, wanawake 93 kati ya 100 waliofunga ndoa ya Kanisani, walisema kuwa wasingekubali kuolewa. Watano walisema wangekubali, wakati wawili waliobaki walisema kuolewa ama kutoolewa kwao yote yalikuwa sawa.
✍️Kwa upande wao kuolewa ama kutoolewa haikuwa tija. Lakini hata wale watano waliokubali walipotakiwa waseme msingi wa kukubali kwao, baadhi ya majibu yao yalisikitisha. Watatu kati yao walisema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuwa Waume zao wanawapenda na ni waaminifu na wakweli katika ndoa zao. “Nathubutu kusema kuwa tangu niolewe, Mume wangu hajawahi kuwa na Mwanamke mwingine. Najua nyendo zake na hanifichi kwa jambo lolote analopanga kufanya ama hata linalomkwaza” anasema Mama mmoja kati ya hao.
✍️Kadhalika, mwingine anasema anajua Mume wake anampenda sana na hajawahi kumtendea jambo lolote la kikatili, hata kule kumsonya tu. “Ninapohisi nimemkosea, hunyamaza na hasira yake ikiisha ndipo huniita na kuniambia kosa langu kwa upole na heshima tena tukiwa wawili tu chumbani. Kwa kweli nampenda sana Mume wangu na najivuna kwamba mimi ni mmoja wa Wanawake waliobarikiwa kupata Mume bora kabisa duniani”
✍️Mmoja anasema, pamoja na Mumewe kuwa mlevi, lakini anampenda kwa sababu hampigi wala kufanya fujo alewapo. Anatunza familia ingawa kama angeacha pombe, wangekuwa na maendeleo makubwa. Wa mwisho ndio alitia fora.
✍️Yeye alisema anafurahia kuishi na Mume wake kwa sababu kila asemacho ama atakacho anatimiziwa bila usumbufu. "Hata nikimwambia naenda kulala kwetu anakubali. Yaani hana shida ingawa watu wanadai eti nimemlisha limbwata, yote naona heri” Lakini anakubali kwamba kama angekuwa anamkatalia mambo anayomuomba, ama kumfanyia vituko vya aina yoyote ile hasa kumpiga, angeshafungasha virago muda mrefu
✍️“Kwa kweli kama kungekuwa na utaratibu wa kila baada ya miaka fulani mtu unarudi tena kanisani na unapewa nafasi ya kuamua upya, naapa hata kwa sumu nisingekubali kuishi na Mwanaume huyu” anasema Mama mmoja katika majibu yake.
✍️Mwingine anasema hata ikitokea Mumewe anafariki na ajitokeze Mwanaume atake kumwoa, hatakubali kuingia tena katika ndoa, labda awe maiti.
✍️Wanawake hawa wanakiri kuteswa kwa namna nyingi na Waume zao na wengine wamepata vilema vya maisha kutokana na kipigo. “Mume wangu amekuwa mlevi na mara nyingi hunigeuza gunia kwa kipigo. Sura yangu imejaa makovu shauri ya kipigo. Sioni maana ya Ndoa wala ule upendo niliotarajia kuupata, sijauona zaidi ya mateso. Kama maana ya Ndoa ndio hii, mie nimeshindwa” anasema Mama mwingine katika majibu yake.
✍️Wengine walisema Waume zao wamewageuzwa kama wafanyakazi wa ndani. Hawathaminiwi, hawana kauli, Waume zao wanalala nje wanavyotaka na wengine wamediriki kuoa Wanawake wengine kinyume kabisa na sheria za Ndoa.
✍️Yote hayo, Mume anayafanya kwa jeuri tu ya kwamba yeye ni mwanaume na hakuna wa kumuuliza.
✍️“Binafsi sijielewi kama mimi ni Mke halali ama Dada wa kazi. Nina mwaka wa nne sijakutana kimwili na Mume wangu. Kila ninapomdadisi, anasingizia ugonjwa ambao hajawahi kuniambia anaumwa nini. Nikija juu anafoka na kusema kama nashindwa kuishi bila kushiriki naye tendo la Ndoa, nitafute Wanaume wengine. Lakini anafanya hivi kwa sababu amepata msichana mdogo anayemchanganya akili” anasema Mama mwingine.
✍️Sababu nyingine, ni tabia ya Wanaume kutowajali Wake zao kiasi kuwa hawajali afya wala uzima wao hata wanapougua.
“Mimi hanijali hata nikiugua. Wakati fulani aliwahi kumleta hapa nyumbani hawara yake huku mimi mwenyewe nikiwa hoi kitandani kwa ugonjwa. Kesho yake wakabebana na huyo mtu wake wakaenda kuishi kwingine. Kama sio ndugu zangu kunichukua na kuniuguza, labda ningeshakufa.
✍️Hapa nimerudi baada ya Wanangu kuniomba sana kwa sababu walikuwa wanaishi maisha ya shida sana.” Hili ni jibu la Mama mwingine aliyeshiriki katika kujibu maswali haya.
✍️Maneno haya na mengine mengi yaliyotolewa na Wanawake hawa, yanathibitisha kuwa Wanawake wengi walioolewa wanaishi katika mazingira magumu ya ndoa.
❤️Ndoa na IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏 MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA adhabu (Waebrania 13: 4)
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz