Naomba nirudie hiki kitu, na ukiona nimeandika jua nina hasira kwakua kuna dada kavunja ndoa yake huko kwa sababu hii hii ya kipumbavu, narudia ya kipumbavu - EDUSPORTSTZ

Latest

Naomba nirudie hiki kitu, na ukiona nimeandika jua nina hasira kwakua kuna dada kavunja ndoa yake huko kwa sababu hii hii ya kipumbavu, narudia ya kipumbavu

by Idd makengo
Naomba nirudie hiki kitu, na ukiona nimeandika jua nina hasira kwakua kuna dada kavunja ndoa yake huko kwa sababu hii hii ya kipumbavu, narudia ya kipumbavu. Umeolewa mume wako ana mtoto nnje ya ndoa, sasa huyo mwanamke aliyezaa nayea anasumbua balaa! Sawa! Anapiga simu mpaka saa nane usiku, kwakua ana kisirani, anaweza hela ya maziwa ya mtoto imeisha, anaweza kukaa mchana kutwa nzima hasemi, saa tisa usiku anapiga simu anaulizia maziwa ya mtoto.
Huyu mwanamke moja kwa moja ni mpweke ana kisirani, wala sina shida naye. Shida ni wewe mke, unaanza kulalamika, unagopmbana na mume wako, unaanza kuweka masharti, unasema sitaki kumuona mtoto, mara unamchkia mpaka mtoto wake. Wewe ndoa yako inakosa amani, mnagombana kiola siku, mume, ndugu wa mume, na ndugu wote wanakuchukia kwakua humpendi mtoto wa mwanamke mwenzako!
Wakati ukiwa bado na kisirani ndoa yako haina amani, yule dada anapata mwanaume, sawa, mwanaume anamuoa, sasa akishaolewa hembu jiulize je ataamka saa nane usiku, aache kupiga shoo na mume wake au amuache mume wake kalala ili kumpigia simu mume wako na kuwakera? Hapana, hakuna mwanaume amabye atavumilia ujinga huo, hata kuongea na mumeo atakatazwa atakua anaongea kwa kificho tena mchana mumewe akiwa kazini.
Sasa wakati yeye anaacha kumsumbua mume wako, wakati yeye ana amani, hakuna tena simu za usiku, hakuna tena maneno maneno, wewe huku ushaharibu ndoa yako, mume anakuchukia kwakua humpendi mtoto wake, wakwe ndiyo kabisa wamekununia na kwako hawaji. Unajikuta hata unaachika, unaondoka na watoto wako, unaenda kuwa single mother unaanza kazi ya kupiga tena simu kama yule mwingine usiku. Kama hujanielewa hapa wewe nunua kitabu changu, soma, nipigie simu ili nikuambie tu “Acha upumbavu unaua ndoa yako kwa mambo ya kijinga!”
makengo
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz