MFANYIE HIVI MKEO KABLA YA KUOMBA MECHI. - EDUSPORTSTZ

Latest

MFANYIE HIVI MKEO KABLA YA KUOMBA MECHI.


Miaka kadhaa baada ya ndoa au wakati fulani katika mahusiano mwanaume unaweza kuona kama mwenza wako haridhiki, unaona kama kazi unayoifanya kitandani haitoshelezi.
Mke au mpenzi wako hatowi ushirikiano na mnapoingia uwanjani unaona kama vile unamlazimisha, hana hamu na wewe na ni kama hakutamani kabisa.
Kwa baadhi ya wanaume hili si tatizo lakini kwa mwanaume anayejua mapenzi hili ni tatizo kubwa na humuathiri mno.
Mapenzi hayana raha kama unafanya na mtu ambaye haridhiki na kuonyesha ushirikiano.
Mwanaume unaweza kuwa unajitahidi, ukifika chumbani unamuandaa vizuri, unafanya kila kitu ambacho unaona wengine wanafanya lakini bado haridhiki na hata unaona kuwa anakusaliti na tatizo nikuwa haridhiki.
Hali hii inaweza kukufanya hata wewe mwanaume kujiona kama vile hutoshi, huwezi kazi na kukupunguzia kujiamini.
Kitu kikubwa ambacho wanaume wengi hawajui nikuwa maandalizi nje ya uwanja ni muhimu kwa mwanamke kama yale ya ndani ya uwanja.
Mke au mpenzi wako haridhiki kwakuwa anaingia kufanya mapenzi na wewe akiwa na mawazo, akiwa anawaza kuhusu watoto, kuhusu michepuko yako, kuhusu tabia zako nyingine za ajabu na kikatili.
Anawaza kuhusu ndugu zako wanavyokuendesha kichwa mpaka ndoa lakini pia ameyazoea maisha yenu yasiyo na mabadiliko mpaka hana raha tena.
Humjali, humnunulii zawadi hata ya mia tano, uko bize na marafiki, unamnyanyasa na kumdhalilisha mbele za watu, uhudumii familia na mambo kama hayo.
Mwanamke kama huyu nilazima atakuwa na hasira na akiwa na hasira basi hatakuwa akifurahia kuwa na wewe kitandani, atakuona kama adui na akili yake haitakuwa sawa.
Kwa mwanamke nilazima awe na furaha ili kufurahia mapenzi zaidi ya hapo utakuwa kama una mbaka tu hata ukijitahidi vipi.
Hivyo basi hebu hakikisha kwanza unampa furaha nje ya uwanja, anza kwa kupunguza na kuacha kabisa kumnyanyasa, mfanye kuwa rafiki yako, afurahie kukupa mwili wake.
Lakini pia mara moja moja hakikisha mnabadilisha uwanja wa mazoezi, mtoe out na fanyia mapenzi sehemu nyingine, sehemu ambayo hatawaza kuhusu kufua mashuka,kupika au kufanya usafi, kichwa chake kiwaze kitu kimoja tu kufurahia tendo la ndoa basiiiii!!!
Sauti iko sawa sawa au inakwaruza?
Deus Mkombozi Kira
Image may contain: flower and text
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz