Mbinu 5 za Kumtokea Mwanaume Yoyote Unayempenda na Kumfanya Wako Milele - EDUSPORTSTZ

Latest

Mbinu 5 za Kumtokea Mwanaume Yoyote Unayempenda na Kumfanya Wako Milele

WANAWAKE wakiwapenda wanaume hubaki na mateso mioyoni mwao. Hii ni kwa sababu ni vigumu kumtokea mwanaume moja kwa moja kumwaga sera kuwa unataka ‘akung’oe’.
Ni kweli kwamba, hata kama mwanaume akimkubali mwanamke awe mpenzi wake baada ya kutokewa, imani yake huwa hafifu kuhusu penzi la kweli la mwanamke huyo. Anaweza kumtumia kwa siku kadhaa kisha akamwacha. Huo ndiyo ukweli.
Wanawake waliowahi kuwatokea wanaume wanaweza kuwa na ushahidi mzuri zaidi juu ya hilo. Pamoja na hayo yote, bado mwanamke anabaki kuwa binadamu, mwenye hisia za upendo na kutamani baadhi ya vitu.
Anaweza kumpenda mwanaume na ni haki yake ya msingi kabisa. Kuwa katika uhusiano na mtu unayempenda kwa dhati ni jambo zuri. Moyo huridhia na kuwa huru katika uhusiano huo.
Hapa katika Team Brayton official love tunakupa dondoo zitakazokusaidia kumsogeza mwanaume ambaye ameuteka moyo wako na hatimaye kuwa wako moja kwa moja. Katika vipengele vilivyotangulia nilieleza kuwa, kwanza mwanamke ni vyema ajitunze na aweke mwonekano wake wenye kuvutia muda wote halafu pia nikaeleza kuhusu kumvutia mwanaume kwa mambo mbalimbali hasa mavazi na mambo anayopendelea.
Sasa tunaanza hivi;
1. ASIWE KWENYE UHUSIANO
Jambo lingine la kuzingatia kwa mwanaume huyo wakati wa harakati za kumweka mikononi mwako ni kuhakikisha hayupo kwenye uhusiano na mtu mwingine. Kuna baadhi ya wanawake wapo tayari kuwa na mwanaume hata kama yupo na mpenzi mwingine; hilo ni kosa na naweza kusema ni umasikini wa kufikiri.
Kama kweli umempenda, itakuwa na maana kama utaweka makazi ya moyo wako kwake milele na siyo kwa muda mfupi tu.
2. JISOGEZE ZAIDI
Tayari umeshakuwa na uhakika kuwa hana mtu, sasa unatakiwa kujisogeza karibu yake. Jizoeshe kumsalimia mara kwa mara na kumsifia kuwa amependeza.
Kamwe usioneshe dalili kwamba wewe ni ‘maharage ya Mbeya’, ishia kwenye kujisogeza karibu yake kwa kumsifia na kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo na siyo zaidi ya hapo.
3. JENGA URAFIKI
Ukaribu wenu sasa unaweza kuwafanya marafiki wa karibu. Kama uko naye ofisi moja au mnaishi mtaa/nyumba moja ni rahisi zaidi. Kuwa rafiki yake wa kweli mwenye kujadiliana naye mambo ya msingi.
Katika urafiki wenu, kamwe usiwe mzungumzaji sana (hasa wa mambo yasiyofaa), aidha usipende kukaa naye katika mazingira yenye vificho ambayo yataweza kusababisha kuingia kwenye mtego mbaya.
4. ZUNGUMZIA ZAIDI MAISHA
Kuzungumzia zaidi maisha na kumshauri juu ya mambo muhimu ya maisha, kutamfanya akuone wewe ni mwanamke makini mwenye malengo mazuri katika maisha yako. Wanaume wanapenda sana wanawake ambao vichwa vyao vinafanya kazi sawasawa.
Hii inaweza kuwa sababu itakayomfanya atamani kuwa karibu yako zaidi, jambo ambalo ndiyo shabaha ya moyo wako.
5. HAKUNA YEYE BILA WEWE
Kwa sababu tayari ni marafiki na mnashirikiana baadhi ya mambo, tengeneza mazingira ya kuwa naye karibu zaidi. Mshirikishe kwenye mambo yako, mfanye ajione si mkamilifu bila kuwa na wewe karibu.
Hili litawezekana kwa kuishika siku yake, kumtakia siku njema na kumjulia hali yake kazini na maendeleo yake kwa ujumla. Kwa kuwa ni marafiki, kwa ndani lazima hisia za mapenzi zitaibuka juu yako na utamuweka kwenye nafasi ya kufikiri kuanzisha uhusiano na wewe.
NI WAKO TU!
Ukipitia hatua zote, bila shaka mwanaume huyo ni wako tu. Ikiwa pamoja na vyote hivyo bado haonyeshi dalili au hajafunguka kuwa unamhitaji, basi mwache, siyo riziki yako.
Kwa nini ung’ang’anie usipopendwa ? Tumia Mbinu Hizi Kumpata Unayempenda na Kumhitaji Kweli.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz