MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO - EDUSPORTSTZ

Latest

MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO

Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO

1. Kila mmoja ana wajibu wa kumheshimu mwenza wake bila kudharauliana.
2. Ni wajibu wa kila mmoja kumsikiliza mwenza wake kwa unyenyekevu na upole.
3. Kila mmoja ana wajibu wa kumfurahisha mwenza wake hasa pale ambapo mwenza wako ana huzuni.
4. Kila mmoja ana wajibu wa kumpenda mwenza wake kwa dhati.
5. Ni wajibu wa wanandoa kila mmoja kumwamini mwenza wake na siyo muda wote kumuwazia mabaya mwenza wako.
6. Ni wajibu wa LAZIMA kila mmoja kuwa na utayari wa kusamehe, maana hii ni nguzo ya maisha ya ndoa.
7. Ni wajibu wa mume na mke kuvumiliana lakini simaanishi kuumizana kwa makusudi kwa sababu unajua mwenza wako atakuvumilia.
8. Ni wajibu wa wanandoa kufundishana na kueleimishana mambo mbalimbali katika ndoa ili kuimarisha ukaribu wa wanandoa.

❤️NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏 MAANA WAASHERATI NA WAZINZI MUNGU ATAWAHUKUMIA ADHABU (WAEBRANIA 13: 4)
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz