Kama amekwambia anakupenda sana na kamwe hawezi kuishi bila wewe basi usiitumie fursa hiyo kumfanyia vituko kwa kuhisi ni kweli hawezi kuishi bila wewe.
Kama amekuonyesha mahaba niue basi usidhani atavumilia hata pale utakapokuwa unamfanyia vituko.
Kuna dhana moja, eti mtu akipendwa sana basi anaanza kufanya baadhi ya vituko ili tu aone unaumia kwa kiasi gani, kiufupi furaha yake ni kukuona unalia kwa ajili tu ya penzi lako.
Zama zimebadilika, siku hizi mtu anampenda yule anayeonyesha mapenzi na heshima. Ukikengeuka tu basi hauna chako, kwani ambapo hukuwa naye unadhani furaha yake aliitoa wapi?
Mtu kukuonyesha mahaba niue isiwe sababu ya kumfanyia vituko bali mpende ikiwezekana hata zaidi ya vile anavyokupenda wewe.
Post a Comment