KATIKA MAISHA YA MAHUSIANO EPUKA MAMBO HAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

KATIKA MAISHA YA MAHUSIANO EPUKA MAMBO HAYA

👉Katika maisha ya mahusiano muepuke sana mtu anaependa kukufananisha na watu wa ajabu ajabu, Muogope sana mtu anaependa kukucompare na watu wenye sifa za kijinga.
👉Mkwepe sana mtu anaependa kukuita majina ya ajabu ajabu, Muogope mtu anaependa kukuona wa kawaida tuu, mtu asieona jipya kwako, mtu asieona thamani yako wala kutambua utu wako.
👉Huyo mtu anakudhihirishia wazi kuwa anakudharau, mtu huyo anakuona wanin, wakazi gan, huna maana. Mtu wa aina hiyo anakuangalia ovyo ovyo tuu, Yupo kwako kwa matumizi yake binafsi lakin wew si chochote, wala si lolote kwake.
👉Jisogeze zaidi kwa mtu anaejua umuhimu wako, mtu anaejua thamani yako, mtu anaejua bila wew yeye sio kitu. Jiweke karibu na mtu anajali utu wako, mtu anaekuthamini.
👉Mpende zaidi mtu anaekuona wew ni wa tofauti katikati ya watu wengine, mtu ambaye hawezi kukufananisha na chochote chini ya anga, yan kutanisha hisia zako kwa mtu anaekuona wew ni bora kuliko bora lolote chini ya jua. Hakika mtu huyo utafika nae mbali kweny safari ya mahusiano.
👉Uzuri na utamu wa mahusiano ni pale unapopata mtu ambae atakuheshimu, atakayekujali, atakayekuelewa, atakayejivunia kuwa na wewe, na atakayekupenda vile jinsi ulivyo.
Ambae atakuwa muaminifu kwako, atakayejua namna ya kukufariji na yule ambaye atakuvumilia bila kukata tamaa licha ya magumu fulani unayopitia.
J4REAL
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz