KABLA HUJAANZA KUWEKA MASHARTI NA MAMBO MENGI UNAYOTAKA KWA MMWANAUME WEKA HADHARANI VITU UTAKAVYOMPA MWANAUME WAKO AFURAHIE UWEPO WAKO KAMA MKE MWEMA..... - EDUSPORTSTZ

Latest

KABLA HUJAANZA KUWEKA MASHARTI NA MAMBO MENGI UNAYOTAKA KWA MMWANAUME WEKA HADHARANI VITU UTAKAVYOMPA MWANAUME WAKO AFURAHIE UWEPO WAKO KAMA MKE MWEMA.....

Image may contain: 1 person, standing
Sio kila siku unasema tu mimi nataka mwanaume mwenye pesa na uwezo wake,kwani hujui kila mwanaume aliyefaninikwa hakosi mwanamke mashuhuri aliyesimama na kupigana nae?
Wewe subiri aliyefanikiwa utadhalilishwa na kunyanyapaliwa kama housegirl badala ya kudekezwa kama malkia aliyechangia mafanikio....
Achana na maneno kwamba bora aloyefanikiwa tayari kuliko mnaepigana nae ataenda kutumia na hawara.....
Ukishindwa kusimama imara kama mke na kuvimba kichwa kwanini usikimbiwe?
Mwanamke mwema hatangulizi maneno ya kujilaani na kujitabiria mabaya piga goti muombee mumeo afanikiwe Mungu atakulindia mpaka atakushirikisha idadi ya wanawake wanaomtongoza au hamjaelewa nguvu ya maombi mliyopewa wanawake ina nguvu ya kuhamisha milima?
Simama imara mwanamke usimamishe nguzo imara ya familia yako acha kutembea na maneno ya wanawake walioshindwa kulinda ndoa kwa kutafuta kushindana na vichwa vyao(waume zao) utabarikiwa mpaka ushangae.....
Huku mitandaoni soma habari za wanaotukana na kubeza ila jifunze kwa walio na hekima,busara na maarifa usibebe kila kitu utambeba shetani na kupoteza mwelekeo wako......
Wanaume na wanawake wema bado wapo pigana utampata na kuishi kwa amani,upendo na furaha......
Mwanamke akisimama imara familia hustawi na kuchanua.
Mwanaume hata angekuwa mkorofi,mkali,mshenzi nk,hawezi kumshinda mwanamke mwerevu na aliyejaa maarifa na hekima ya KIMUNGU....
Ukipiga goti na kulia tu utamkomboa mumeo na uzao wenu,fanyika baraka kwa mumeo usiwe sehemu ya kimpoteza zaidi.
Ulifanywa kuwa ubavu wake timiza wajibu wako acha kabisa kumdhihaki na kumtukana huyo ndio chaguo lako..........!
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz