IJUE TOFAUTI KATI YA MWANAUME NA MVULANA - EDUSPORTSTZ

Latest

IJUE TOFAUTI KATI YA MWANAUME NA MVULANA

Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO
Uanaume sio kutembea na wanawake rundo, ila huo ni uvulana, unaume ni kulinda hisia za mtu kwa kutoanzisha mahusiano ambayo unajua hauko tayari kuyapeleka Mpaka mwisho. Hata kama msichana ameonesha kukupenda kwa upendo mkubwa sana, jukumu lako kama mwanaume ni kulinda hisia zake.
Kama unaona kabisa wewe na yeye hamuendani ya nini kuendeleza mawasiliano ya karibu?
Eti "Naogopa kumuumiza" sasa kwa kuwa na mtu wakati unajua humpendi wala huna nia naye si ndio maumivu makali zaidi kuliko ungemwambia ukweli?
Ukiusema ukweli mapema unasaidia kuliko ukiuficha Mpaka ukaja kujitokeza baadae. Usimdanganye danganye, mwambie ukweli ajue pakushika kuliko kumpa matumaini yasiyokuwepo.
Na hii tabia ya kuanzisha mahusiano mapya wakati upo kwenye mahusiano mengine na hamjaachana eti unamuweka mtu on hold ili huku pakizingua unahamia upande wa pili hilo nalo ni pepo la Mitala.
Hizo tabia unafanya Leo kwenye mahusiano ndio huwa zinaota mizizi na baadae zinatokea hata kwenye Ndoa. Kama ukigombana na mwanamke unatafuta mtu wa kupotezea mawazo, kesho utagombana na mkeo utatafuta kamchepuko. Mazoea hujenga tabia.
Anza kuwa mwanaume kwa kuwa responsible ukijali hisia za wengine. Mungu anakuona unavyoliza watoto wa watu.
Sio sifa wala nini bali ni upuuzi mtupu na nichukizo kwa Mungu.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz