Haya ndio maswali ya kujiuliza pale mnaporudisha mahusiano wewe na mpenzi wako. - EDUSPORTSTZ

Latest

Haya ndio maswali ya kujiuliza pale mnaporudisha mahusiano wewe na mpenzi wako.Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO

Kitendo cha kuachana na baadae kurudiana siyo kosa na ni hatua nzuri zaidi ya kujifunza mlipokuwa mmekosea.
Mpaka kufikia hatua ya kurudiana maana yake kuna mmojawapo ameleta hoja na nia ya kutaka kuurudisha uhusiano huo au kuna mtu amekuwa kiunganishi cha kutaka mrudiane,anaweza kuwa mtoto mliezaa au rafiki,ndugu au na wengineo...
Zipo sababu nyingi zinaweza kuwafanya mrudiane japo mlikuwa mmeachana muda mrefu..
Lakini kabla hujafanya maamzi hayo lazima ujiulize maswali yafuatayo:
Endelea kunifatilia ili kuyajua maswali hayo ya kujiuliza

*Swali  la kujiuliza pindi mnaporudisha mahusiano wewe na mpenzi wako.

Swali 1
Je, kwanini anataka mrudiane tena?
Ni vigumu sana kujua nia yake ya kutaka kurudiana,huenda kuna vitu alikuwa anapata kutoka kwako amevikosa huko alipokuwa amekimbilia,
Lakin pia huenda huko amepigwa chini ,au tabia za huyo alipokimbilia anaona bora ya zako,au kuna kitu anataka kulipa kisasi kwako au kukufanyia kibaya dhidi ya huyu ulienae ili umkose,au huenda kweli mwanzoni alipitiwa amekuja kwa nia ya dhati au kashauriwa na watu.
Yote haya ni ya kujiuliza na yanawezekana...

Swali 2
Je, ni kipi kilisababisha mwanzoni mkaachana?
Hili pia ni swali la msingi ili ufanye ulinganifu kama kweli ilikuwa sababu ya msingi kwake kukuacha. Mfano, kama alikuacha kwa kufumania SMS ya mapenzi kwenye simu yako, je, akija kuifumania tena kwa bahati mbaya na penyewe atakuacha?
Sababu iliyowaachanisha mwanzoni ifanyiwe ulinganifu .
Kwa leo niishie hapo swali la 3 na 4 tukutane wakati ujao..........
Endelea kunifatilia.

3. Je, ni madhara gani yalikupata kipindi anakuacha?
Huenda kuna vitu mlikuwa mmefanya kwa maendeleo yenu hatimae vikasambaratika kwa sababu ya kuachana,uliumia,ulidhalilika,ulijutia muda uliopoteza wakati wa mahusiano yenu.
hayo yote yatazame...

4. Mlipoachana hapo kati kati amekutana na wangapi na kwann ameachana nao?
Kumbuka nae kama binadamu mlipoachana huenda aliingia kwenye mahusiano mapya,jiulize hao alioanzisha nao mahusiano wako wapi?

Baada ya kujiuliza maswali yote hayo iruhusu akili yako ifanye maamuzi yatakayofaa kwa usalama wa moyo wako...
*Endelea kunifatilia ili kuyajua Madhara utakayoyapata pindi mnaporudisha mahusiano wewe na mpenzi wako.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz