HAYA MAMBO NDIO HUFANYA VIJANA TUONE KUOA NI MZIGO - EDUSPORTSTZ

Latest

HAYA MAMBO NDIO HUFANYA VIJANA TUONE KUOA NI MZIGO

Habari wandugu kwa ujumla? Nadhani kuna wengine wana maumivu na wengine wanafurahia ndoa yao.
Kwanza kabisa natoa shukurani kwa Mshana Jr kwa uzi wako mkuu huu Ule msimu umeanza tena nimeupenda sana,umeelewa mambo flani ambayo laiti kama kila mwenye shida izo angachukua hatua angeona manufaa.
LEO NAPENDA KUONGEZEA MTAZAMO WANGU KUHUSU KUVUNJIKA KWA MAHUSIANO MENGI
Jambo la kwanza kabisa katika jamii shetani amewafanya watu waone ngono ni jambo la kawaida sana kwa kila mtu tofauti na zamani.
Kuna msemo vijana kama Zero IQ wanautumia eti "
Daima sahau kuoa.
yan ni kawaida kwa vijana kuchuana na kuishi bila mipango yeyote,ili mradi tu kutimiziana haja zao. Upendo wa kweli utatoka wapi hapo?
USHAURI KWA VIJANA
Bado hujachelewa,iwe umeumizwa au bado hujaamua kutafuta mwenzi wako.
1. Ili ufaidike na ndoa hakikisha unaachana na dhambi ya zinaa/uasherati
2. Chagua mtu anaemwogopa Mungu kuliko wewe,sababu ataƓgopa hata afanyacho sirini
3. Weka lengo la muda mrefu,usioe kisa rafiki yako kaoa(usifuate mkumbo)
4. Usioe kwa kushinikizwa na ndugu, marafiki. Panga mwenyewe(kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe)
5. Usifanye ngono na mchumba/rafiki yako ulie mtarget
6. Tumia muda(sio siku wala miezi) kumjua utakayempata ana mapendezi gani?
7. Penda kuwa nae karibu lakini sehem za wazi(au awepo na mtu mwingine)
Kama utaweza kuwa na huo usmat hata wanawake wenyewe watakuwa wanakutafuta wewe,sababu wanapenda wanaume wenye kujali na wenye malengo.
UKISHAOA SASA
Mwamuzi wenu ni neno la Mungu yan Biblia/Quran, sio kila mtu mana kuna wengine hawapendi mnavyoishi
1. Acha kabisa kufikiria makoloni yako ya zamani (mkazie fikra mwenzi wako unapokua mbali nae)
2. Usiogope kuwa muwazi kwa kila jambo ili ajue unapenda nini na nini hupendi.
3. Matatizo ni yenu wawili tu wengine hawayawahusu.
4. Kila mmoja awe msikivu kwa mwenzake.
Mkizidiwa mtafute kiongozi wako wa dini mwenye busara na hekima omba muongozo kwake.
Mwenye nyongeza aongezee hapo




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz