MODRIC ANASTAHILI KUSHINDA TUZO YOYOTE ZAIDI YA MESSI-RAKITIC - EDUSPORTSTZ

Latest

MODRIC ANASTAHILI KUSHINDA TUZO YOYOTE ZAIDI YA MESSI-RAKITIC


Msimu huu Messi ametumbukiwa nyongo baada ya kukatwa kila tuzo asipate hata kuingia hatua za mwisho

Kiungo wa Barcelona Ivan Rakitic anaamini Lionel Messi hawezi kushinda tuzo yoyote msimu huu kwani ni lazima itaende kwa nahodha wa timu yake ya taifa ya Croatia Luka Modric.

Modric ambaye katoka kushinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya Kombe la Dunia ya Golden Ball baada ya kuongoza taifa lake la Croatia, Modric aliitwa Mchezaji wa Mwaka wa UEFA na ni mgombea wa tuzo ya mchezaji bora kwa upande wa Wanaume wa FIFA.

Messi alipoteza nafasi ya kuchaguliwa, na mchezaji wa Real Madrid amepigana na Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah kwenye tuzo.

Rakitic anaamini Modric anastahili tuzo bora, na heshima nyingine yoyote na mchezaji wake wa timu ya Barcelona Messi hawezi kushinda.
"Kama kuna tuzo ya pekee ambayo Lionel Messi hawezi kushinda, basi hakuna shaka kwamba msimu huu inapaswa kwenda kwa Luka Modric," aliiambia Marca.

"Haikuwa kushangaza kwangu kama angeweza kushinda na kura nyingi zaidi. Huu umekuwa mwaka wake na nina furaha sana kwa ajili yake.
"Kama Messi sio bora, basi lazima iwe Modric."

Pamoja na kuiongoza Croatia katika fainali ya Kombe la Dunia, Modric alisaidia Madrid kushinda Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz