MBAPPE AZIDI KUITEKA REAL MADRID KUELEKEA PENGO LA CR7 - EDUSPORTSTZ

Latest

MBAPPE AZIDI KUITEKA REAL MADRID KUELEKEA PENGO LA CR7

Mbappe anaen­delea kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaowaniwa kwa uka­ribu na wababe wa Ulaya,Madrid walio na pengo kubwa la cr7
Mbappe 

 Mbappe anaen­delea kutajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaow aniwa kwa uka­ribu na wababe wa Ulaya, Real Madrid licha ya mche­zaji huyo kusisi­tiza kuwa hana mpango wa ku­hama kutoka Paris Saint-Ger­main (PSG) kwa sasa.

Mbappe mwenye miaka 19 alifunga goli la nne la Ufaransa walipoichapa Croatia 4-2 fanali ya Kombe la Dunia Moscow, pamoja na kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo katika michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Paris St-Germain Mbappe ndiye mchezaji wa pili asiyetimiza miaka 20 kutikisa wavu kwenye fainali ya Kombe la Dunia tangu Pele mnamo 1958.

Mbappe al­ionyesha kiwango cha juu akiwa na Ufaransa ka­tika Kombe la Dunia na kui­wezesha timu hiyo kubeba ubingwa, ame­kuwa akipigi­wa debe kwa kiasi kikubwa k u s a j i l i w a na kuoneka­na anafaa kuibeba Ma­drid baada ya kuondoka kwa Ronaldo.

Tangu Kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kwenda Juventus, Madrid au Los Blancos wamekuwa wakipambana sokoni kuhakikisha wanafanya usajili wa staa mkubwa kama ili­vyo kawaida yao kwa ajili ya kuziba pengo hilo.

Taarifa za ndani ya Madrid zi­naeleza kuwa Mbappe ambaye ana umri wa miaka 19 bado anaoneka­na kuwa ni chaguo sahihi na ndiyo maana mabosi wanahaha kuhak­ikisha wanalifanikisha hilo.

Mbappe anazidi kupata Sifa  nyingi ambazo zi­nambeba chipukizi huyo kusajiliwa ikiwemo kuonyesha makali akiwa na umri mdogo kuanzia ngazi ya klabu hadi timu ya taifa.

Kingine kuhusu Mbappe ni uwezo wake wa kufun­ga, amekuwa akionyesha makali katika ufungaji licha ya kuwa siyo straika halisi, kazi yake imekuwa nzuri licha ya kuwa amekuwa kati­ka kikosi kimoja na mastraika halisi wenye uwezo wa juu.

Hiyo inanogesha kwa kuwa in­aonekana kama anafuata nyayo za Ronaldo ambaye naye alikuwa winga lakini mwenye uwezo mkubwa wa kufunga.

Kibiashara pia nyota huyo anaonekana kuwa vizuri kwa kuwa hadi sasa sura yake imekuwa na soko kubwa PSG, hivyo upande mwingine Madrid wanaamini bi­ashara itakuwepo wakimsajili.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz