KLABU YA SIMBA YAWAHURUMIA WAKIMATAIFA - EDUSPORTSTZ

Latest

KLABU YA SIMBA YAWAHURUMIA WAKIMATAIFA

klabu ya  Simba sc sa  kupitia kwa kaimu Makamu wake wa Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ imesema kuwa haiwezi kusajili mchezaji yoyote kutoka klabu ya Yanga
Klabu ya simba waihurumia yanga

Klabu ya  Simba sc kupitia kwa kaimu Makamu wake wa Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ imesema kuwa haiwezi kusajili mchezaji yoyote kutoka klabu ya Yanga kwa sasa kwakuwa inafahamu hali ngumu inayoikumba klabu hiyo.

Inafahamika kuwa siku za karibuni kumekuwa na tetesi za klabu Simba kutaka kumsajili mchezaji Kelvin Yondani kutoka kwa mahasimu wao baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu uliokwisha.

Baada ya tetesi hizo kusambaa ndipo uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuinusuru klabu hiyo, Abbas Tarimba walipokutana na Yondani na kumalizana naye kwaajili ya kuendelea kucheza msimu ujao.

Timu ya simba sc kupitia makamu wake maarufu kama  , Try Again amesema kuwa Yondani ni mchezaji Tegemeo wa Yanga na endapo klabu Simba ikimsajili manaake wataibomoa klabu hiyo na itakuwa haijengi mpira wa Tanzania akilinganisha na usajili wa msimu uliokwisha wa Haruna Niyonzima na Ibrahim Ajibu kwa klabu hizo.

“ Tunafahamu Yanga wako kwenye matatizo, na hali ngumu sasa tunapoendelea kuwabomoa hatuusaidii mpira bali tunaudidimiza mpira “. Amesema Salim Abdallah

 Klabu ya Simba msimu uliopita ilimsajili Haruna Niyonzima kutoka Yanga na Yanga ilimsajili Ibrahim Ajibu kutoka Simba wakiwa na mategemeo makubwa ya kufanya vizuri katika ligi lakini wachezaji hao wakuweza kuzisaidia klabu zao kwa kiwango ambacho kilitarajiwa.

Ajib alimaliza msimu akiwa na magoli 7 pekee huku Haruna Niyonzima akicheza katika mzunguko wa kwanza wa ligi pekee baada ya kuumia katika mzunguko wa pili

chanzo eatv


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz