KAKAMEGA YAMMEGA YANGA HUKU WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHUHUDIA - EDUSPORTSTZ

Latest

KAKAMEGA YAMMEGA YANGA HUKU WACHEZAJI WA SIMBA WAKISHUHUDIA


Kikosi cha simbaWachezaji wa kikosi cha Simba wakiongozwa na Kocha Msaidizi wa timu, Masoud Djuma, leo walikuwa Uwanjani kuishuhudia Yanga ikicheza dhidi ya Kakamega Boys.


Katika mchezo huo ambao Yanga imekubali kufungwa mabao 3-1 na kuondolewa kwenye mashindano hayo ya SportPesa Super CUP, Simba walipata nafasi ya kuutazama mchezo huo ili kuzisoma timu zote mbili.

Simba watashuka dimbani kesho Jumatatu kucheza dhidi ya Kariobang Sharks, mchezo ukianza majira ya saa 9 alasiri.

Wakati huo wachezaji Shiza Kichuya na Mohamed Rashid wameondoka pamoja leo kuelekea Nakuru ili kujiunga na kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano hayo.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz