ALICHOZUNGUMZA HAJI MANARA BAADA YA YANGA KUCHEZEA KICHAPO CHA 3-1 - EDUSPORTSTZ

Latest

ALICHOZUNGUMZA HAJI MANARA BAADA YA YANGA KUCHEZEA KICHAPO CHA 3-1Haji Manara

Baada ya Yanga kuondoshwa katika mashindano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya na Kakamega HomeBoys, Ofisa wa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa Yanga wamewakimbia makusudi.

Yanga imeagwa rasmi kwenye michuano hiyo kwa kukubali kichapo cha mabao 3-1, mchezo ukipigwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Kufuatia kichapo hicho, Manara amefunguka na kueleza kuwa Yanga wamefanya makusudi sababu akieleza kuwa wanaogopa kukutana na Simba.

Manara ambaye timu yake inashuka dimbani leo saa 9 alasiri kucheza na Kariobang Sharks, amesema kuwa Yanga wametolewa na timu ndogo tofauti na vile ambavyo amekuwa ametarajia.

Akizungumza kupitia Radio EFM katika kipindi cha E Sports, Manara ameeleza hayo huku akisema wao wamejiandaa kupigania kikombe ili kucheza na Everton huko Goodison Park, England.

Mbali na Yanga kuyaaga mashindano, JKU nayo pia imeunga tela kwa kukubali kupoteza dhidi ya Gor Mahia FC kwa jumla ya mabao 3-0.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz