HILI NDILO JAMBO WALILOOMBWA UONGOZI WA YANGA KUIGA KUTOKA SIMBA - EDUSPORTSTZ

Latest

HILI NDILO JAMBO WALILOOMBWA UONGOZI WA YANGA KUIGA KUTOKA SIMBA

Jengo la club ya yanga

Kufuatia kushindwa kufanya hivi karibuni na licha ya kikosi cha Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa ligi uliopigwa jana Uwanja wa Taifa, mashabiki Yanga wameutaka uongozi wao kufanya mabadiliko.

Mapema baada ya mchezo dhidi ya Mbao kumalizika, baadhi ya wapenzi, mashabiki na wanachama walitoa maoni yao kuhusiana na mwenendo wa kikosi cha Yanga wakieleza ni vema Yanga ikaiga walichofanya Simba.

Wengi walieleza ni wakati mwafaka sasa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa klabu hiyo ili kuepukana na kuyumba kwa uchumi, suala ambalo klabu inalipitia kwa sasa.

Mbali na hilo mashabiki hao wameeleza kuwa mfumo uliopo hivi sasa umesababisha Yanga kuwa na matatizo haya yanayoikumba hivi sasa haswa ukata wa fedha huku wakishauri ni muda sahihi kuondokana nao.

Wakati mashabiki hao wakitoa maoni hayo, watani zao wa jadi Simba tayari wameshakamilisha mchakato mzima na kilichosalia hivi sasa ni usajili wa katiba na uwezekano mkubwa wa mfumo huo kuanza kutumika upo kabla ya msimu ujao wa ligi kuanza.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:

Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz