WANAOTAJWA KUMRITHI ARSENE WENGER HAWA HAPA - EDUSPORTSTZ

Latest

WANAOTAJWA KUMRITHI ARSENE WENGER HAWA HAPA


Meneja mpya wa Arsenal kujulikana kabla ya kombe la dunia


Arsene Wenger atahitimisha miaka 22 ya kuiongoza Arsenal Mei 13


Klabu ya soka ya Arsenal inauhakika wa kumtangaza meneja mpya wa timu hiyo atakayechukua mikoba ya Arsene Wenger, kabla ya kuanza kwa fainali za michuano ya kombe la dunia.

Washika mitutu hao wa London,hawajaweka hadharani lini itakuwa muda rasmi wa mwisho wa kusaka meneja mpya, lakini meneja mpya atajulikana kabla ya tarehe 14 Juni , tarehe ambayo michuano ya kombe la dunia itakuwa inaanza kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique

Wenger aliyedumu katika klabu ya Arsenal kwa miaka 22, ataingoza timu hiyo katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kumalizika kwa ligi jumapili ya Mei 13.

Meneja wa zamani wa Fc Barcelona Luis Enrique, anatajwa kuwa miongoni makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua kazi za kuinoa Arsenal pia yupo meneja wa Juventus Massimiliano Allegri.

Pia viungo wawili wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta ambae kwa sasa ni Kocha msaidizi wa Manchester City na Patrick Viera, anayekinoa kikosi cha New York City, pia wanapigiwa chapuo ya kupewa kazi hiyo.

Makocha wengine anaotajwa sana kuweza kuinoa Arsenal ni kocha wa Monaco Leonardo Jardim na Carlo Ancelotti.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz