TETESI ZA SOKA LA ULAYA LEO 08.05.2018 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD EDUSPORTSTS NEWS APP HAPA

Tuesday, 8 May 2018

TETESI ZA SOKA LA ULAYA LEO 08.05.2018


Meneja wa Hudderfield David Wagner


Leicester inamtaka meneja wa Hudderfield David Wagner kuwa mkufunzi wao mpya , Foxes wanatarajia kumuaga meneja wao Claude Puel mwezi huu. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard ,27, amesema ''hana nafasi'' ya kuondoka Stamford Bridge kuelekea Manchester United. (Mail)

Wenger: Nitawakosa sana mashabiki wa Arsenal

Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata , 25, ana uwezekano wa kurudi Juventus na Chelsea wanaweza kufikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani , 31. (Tuttosport, via Metro)Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal

Arsenal inamtaka meneja wa Juventus Massimiliano Allegri au kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa mkufunzi wao mpya, lakini wawili hao bado wanawasiwasi kuhusiana na uongozi wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Enrique yuko katika hali ya kutaka kiwango kikubwa cha malipo yake iwapo atakuwa meneja mpya wa Arsenal- baada ya kutaka kulipwa £15m baada ya kukatwa ushuru. (Mirror)

Man City yakabidhiwa kombe la ligi kuu ya England

Meneja wa Napoli Maurizio Sarri ambaye amehusishwa na Chelsea ametoa pendekezo la kuiaga upande wa klabu hiyo ya Serie A wakati wa majira ya joto iwapo atadhibitisha kuna kifungu cha kutolewa kwa yuro milioni 8 katika mkataba wake. (Talksport)

Liverpool imezungumza na Juventus kuhusu mkataba wa Sami Khedira mwenye umri wa miaka 31 wakati wa uhamisho wa bure kwa kiungo wenzake Mjerumani Emre Can, 24, kuelekea upande wa Italia. (Sun)

Bayern Munich wako tayari kumuuza mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski, 29, anayetegewa na Manchester United. (Calciomercato, via Express)Kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta

Kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta pendekezo lake la uhamisho kuelekea kwenye Ligi Kuu ya Uchina inaweza kuwa na shaka baada ya Chongqing Lifan kudokeza mkataba wa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 33 unaweza kusitishwa kutokana na matatizo ya kifedha. (Goal.com)

Kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves anatarajia kuichezea klabu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi kuu ya Uingereza licha ya mitizamo tofauti kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa kimataifa. (Guardian)

Diego Costa awazuia Arsenal kufika fainali Europa League

Mlinda lango wa Uhispania Iker Casillas, 36, anaweza kusalia na klabu ya Porto kwa msimu mwengine baada ya kushinda taji lake la kwanza na klabu ya Ureno msimu huu. (Marca)

Mkufunzi wa Southampton Mark Highes anazidi kupata uugwaji mkono na wachezaji katika uwanja wa St Mary kuendelea kuiongoza klabu hiyo licha ya kuwa katika kiwango cha hatua ya kushushwa daraja mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

Mmiliki wa klabu ya Bristol City Stephen Lansdown amesema hana ufahamu wowote iwapo mkufunzi wa klabu hiyo Lee Johnson amehusishwa na klabu ya West Brom. (Birmingham Mail)Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionMshambuliaji wa Manchester United na Ubeligiji Romelu Lukaku

Mshambuliaji wa Manchester United na Ubeligiji Romelu Lukaku , 24, amesema jeraha lake la kifundo cha mguu linaendelea vizuri ''kinyume na matarajio yake.'' (Manchester Evening News)

Tiketi za mechi kati ya Huddersfield dhidi ya Arsenal, ambayo ni mechi ya mwisho ya Arsene Wenger kwa the Gunners , zinauzwa kwa zaidi ya £200- licha ya onyo kwa mashabiki ''kunyanyaswa.'' (Huddersfield Daily Examiner)

Meneja wa Brighton Chris Hughton anatarajia uhamisho mwenye utaratibu kuliko wa msimu uliopita wa majira ya joto ambapo wachezaji saba walisajiliwa - sasa klabu hiyo imedhibiti wadfa yake kwenye ligi kuu Uingereza. (Argus)
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ