UTATA ALIOUACHA DONALD NGOMA YANGA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 27 May 2018

UTATA ALIOUACHA DONALD NGOMA YANGA

Donald ndombo ngoma mchezaji wa zamani wa yanga amesaini mkataba wa wa awali wa mwaka mmoja na klabu ya azam.


 Ngoma ni miongoni mwa wachezaji waliochangia mafanikio ya yanga kwa miaka 3 mfululizo kwenye ligi kuu Tz bara. akiwa amesajiliwa kutoka katika klabu ya Fc platnum ya kule zimbabwe.

 Lakini hali ilianza kubadilika kwa mchezaji huyo baada ya kuwa na majeraha ya muda mrefu na alilazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda wa msimu mzima sasa. 

Huku mara kadhaa akichelewa hata kurudi kambini kuungana na wenzake kwa makosa ya kinidhamu.

 Ngoma alikuwa analipwa zaidi ya milioni 6 kwenye klabu ya yanga lakini mashabiki walikuwa hawaliziki na mwendendo wake katika kuisaidia timu. 

 wakati msimu ukifika ukingoni uongozi wa yanga ulikubali kuvunja mkataba nae na rasmi amesajiliwa na azam ambao wamesema watamlipia matibabu mpaka awe sawa ndio waanze kumtumia katika msimu ujao. 

 Utata unakuja kweli yanga walishindwa kumhudumia ngoma kwa majeraha yake na mara kadhaa alionekana anatolewa taarifa kwamba yupo kwao kwa matibabu?, Au alikuwa hayupo tayari kucheza yanga kwa maslahi yake?. 

 Mashabiki wa yanga wamepokea taarifa hiyo kwa furaha tofauti na wachezaji wengine walipoondoka kama Haruna niyonzima, lakini kwa upande wao imekuwa furaha sababu wanaamini ni moja wa wachezaji waliokwamisha juhudi zao msimu huu.