RONALDO AZUA UTATA MPYA REAL MADRID - EDUSPORTSTZ

Latest

RONALDO AZUA UTATA MPYA REAL MADRID


Mchezaji nyota wa Real madrid Christiano Ronaldo amezua utata mpya ndani ya klabu na pengine akapunguza furaha ya mashabiki wa madrid baada ya kushinda fainali ya champions league.

Ronaldo katika mahojiano yake mjini kyiv siku ya jumamos baada ya fainali alisema
" nitatangaza hatma yangu ndani ya muda mfupi kuhusu maisha yangu ndani ya madrid".

Kauli ambayo inaashilia kwamba anaweza kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kuweka historia nyingi na heshima kubwa ndani ya klabu hiyo.

Baada ya taarifa hiyo kapteni wa Real madrid sergio Ramos alisema Ronaldo anatakiwa kuweka sawa taarifa hiyo kwa mashabiki wa Real madrid".

Lakini wanamichezo wengi ni watu wenye mbinu nyingi pale wanapotaka kuongezewewa maslahi yao si mara ya kwanza kumskia Ronaldo akisema hivyo


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz