REFA ATAKAYECHEZESHA FAINALI YA REAL MADRID NA LIVERPOOL - EDUSPORTSTZ

Latest

REFA ATAKAYECHEZESHA FAINALI YA REAL MADRID NA LIVERPOOL


Mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kwa sasa ni fainali ya
klabu bingwa barani Ulaya ambayo itawakutanisha Real Madrid na Liverpool Jumamosi ya Mei 26 mwaka huu.

Tayari kamati ya waamuzi ya UEFA imemchagua mwamuzi wa kati ambaye anachezesha mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa NSC Olimpiyskiy, Kyiv kwa kusimamia sheria 17 za soka.

Kamati hiyo imemteua Milorad Mažić kutoka nchini Serbia kuchezesha fainali hiyo ambayo inataajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili.

Mažić, 45, amekuwa mwamuzi wa kimataifa tangu 2009 na amewahi kuchezsha fainali kadhaa ikiwemo ile ya mabara mwaka jana iliyowakutanisha Chile and Germany, UEFA Super Cup 2016 kati ya Real Madrid na Sevilla.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz