RATIBA YA LIGI KUU YAPANGULIWA NA TFF - EDUSPORTSTZ

Latest

RATIBA YA LIGI KUU YAPANGULIWA NA TFFShirikisho la soka nchini kupitia kwa Bodi ya ligi (TPLB), limepangua mchezo wa ligi kuu soka
Tanzania bara kati ya Mbao FC na Ndanda FC uliokuwa unatarajiwa kucheza Ijumaa ijayo.

Taarifa ya TFF leo, imeeleza kuwa mchezo huo umerudishwa nyuma kwa siku moja ambapo badala ya kuchezwa Ijumaa sasa utachezwa Alhamisi ya wiki hii sababu kubwa ikiwa ni uwanja kuwa na shughuli nyingine.

''Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Mbao FC ya Mwanza na Ndanda FC ya Mtwara uliokua uchezwe Mei 11, 2018 umerudishwa nyuma utachezwa Mei 10, 2018 Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, kufuatia Uwanja huo kuwa na matumizi mengine ya kijamii'', imeeleza taarifa hiyo.

Mbao FC inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu kwenye mechi 26 ilizocheza huku ikiendelea kuwa kwenye mstari wa kushuka daraja. Ndanda nayo ipo nafasi ya 15 ikiwa na alama 22 baada ya mechi 27.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz