Type something and hit enter

By On
Rais Trump wa Marekani
Rais Trump amekubali rasmi kwamba alimlipia mwanasheria wake binafsi zaidi ya dola laki moja

katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Maadili ya Serikali ya Marekani, haielezei sababu ya malipo kwa Michael Cohen mwaka jana ingawa kuna maelezo kidogo tu imeainishwa kama gharama.

Bwana Cohen, hata hivyo, amekubali kulipa zaidi ya dola laki moja na thelathini kwa nyota wa masuala ya ngono Stormy Daniels muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu wa Uraisi mnamo mwaka 2016.Stormy anadai aliwahi kuwa na uhusiano na bwana Trump mnamo mwaka 2006 ,na walikutana katika hoteli ya Lake Tahoe

Stormy anaeleza kuwa alilipwa kiasi hicho ili kumziba mdomo kuhusiana na kuwepo na tuhuma za uhusiano baina yake na bwana Trump na inajitokeza sasa kinyume na makubaliano ya awali.

Majaribio ya farasi na kucheza na mbwa . Stormy Daniels ni mwigizaji wa filamu maarufu na aliwahi kushinda tuzo na ambaye amepitukia kwenye sekta masuala ya ngono kama haitoshi sasa anajitoma katika siasa taratibu

Mnamo mwezi Aprili, raisi Trump alisema hakumbuki kama bwana Cohen alikuwa amemlipa Bi Daniels kabla ya uchaguzi wa 2016. Malipo ya Trump kwa Cohen mara ya kwanza alithibitishwa na Rudy Giuliani, ambaye ni mmoja wa mawakili wa rais katika mahojiano ya televisheni.

Bwana Giuliani anasema shughuli hiyo ilikuwa na kazi moja tu kumnyamazisha bi Daniels kuhusu "mashtaka ya uwongo na ya udanganyifu" kwamba alifanya ngono na Trump, lengo likiwa ni kumsafisha mgombea nafasi ya uraisi wa wakati huo ambaye sasa ni raisi wa Marekani.

Baadaye wiki hiyo hiyo, raisi alisema Bwana Giuliani aliyekodiwa alihitaji muda wa kukusanya taarifa za ukweli mtupu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ
Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako Utasoma habari zote hata kama hauna MB

Click to comment