TETESI ZA USAJILI NA SOKA LEO MAY 17 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Thursday, 17 May 2018

TETESI ZA USAJILI NA SOKA LEO MAY 17


Nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira, 41, anasema amekasirishwa msh ahara ulionukuliwa na klabu hiyo baaada ya kuzungumziwa kuhusu nafasi ya umeneja iliyo wazi. (Sky Sports)


Manchester United wana uhakika wa kumsaini mlinzi Toby Alderweireld, 29, kutoka Tottenham. Red Devils wana nia ya kutumia pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji. (Evening Standard)

West Ham watazungumza na meneja wa Newcastle Rafael Benitez, huku naye meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca kuwa miongoni kwa wale wanatafutwa. (Mirror)

Manchester United wanakaribia kumaliza makubaliano ya pauni milioni 43.7 na beki wa Juventus Mbrazili Alex Sandro, 27, huku mlinzi raia wa Italia Matteo Darmian, 28, akitarajia kuhamia Manchester United. (Le Stampa via Football Italia)

Wolves na Monaco wanammezea mate mshambulizi wa AC Milan raia wa Ureno Andre Silva, 22, ambaye alijiunga na Rossoneri kwa pauni milioni 33 msimu uliopita. (Sky Sports Italy - in Italian)

Kikosi kitakachoibeba Brazil Kombe la Dunia chatajwa
Arsenal wameanza kumtafuta mlinzi wa Borussia Dortmund raia wa Ugiriki Sokratis Papastathopoulos, 29, ambaye wanaamini kuwa watamsaini kwa pauni milioni 17.5 baada ya kuacha kumwinda raia wa Uturuki Caglar Soyuncu ambaye thamani yake ilitangazwa kuwa pauni milioni 35. (Mail)

Arsenal pia wana mpango wa kumsaini mlinzi raia wa Ireland Kaskazini Jonny Evans kwa pauni milioni 3 kufuatia kuzushwa kwa West Brom. (Mirror)

Mlinzi wa Stoke mwenye umri wa miaka 25 Kevin Wimmer, aliyesainiwa kutoka Tottenham kwa pauni milioni 18m msimu uliopia yuko kwenye mazungumzo kuhusu kuhamia klabu ya Ujerumani ya Hannover. (Mail)

Mchezaji wa Hull City Abel Hernandez, 27, anaweza kuhamia Leeds wakati mkataba wake utamalizika baadaye msimu huu. (Yorkshire Evening Post)

Mlinzi wa Celtic Kieran Tierney, 20, anakiri kuwa anawindwa na Atletico Madrid lakini amedai atasalia Celtic hadi mwisho wa taaluma yake. (Herald)

Atletico Madrid washinda Europa League
Mchezaji wa Chelesea raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema anasubiri kuona mazungumzo na Chelsea kanbla ya kusaini mkataba mpya. (Independent)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino yuko tayari kuwakataa Chelsea kwa sababu anasema ana furaha kuwa na klabu yake. (Star)

Arsenal wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Nice Jean-Michael, 26, ambaye thamani yake ni pauni milioni 40. Lakini mahasimu wao wa London Chelsea wanaongoza mbio na kumsaini raia huyo wa Ivory Coast. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mikel Arteta, 36 anakaribia kuwa meneja mpya wa Arsenal akichukua nafasi ya Arsene Wenger baada ya mazungumzo kuendelea kati ya pande hizo mbili. (Independent)


EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ