MAJERAHA MAKUBWA KUWAHI KUTOKEA LIGI KUBWA 5 BARANI ULAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

MAJERAHA MAKUBWA KUWAHI KUTOKEA LIGI KUBWA 5 BARANI ULAYA

Hivi unawajua wachezaji waliowahi kupata majeraha makubwa na kukaa nje siku nyingi pia kukosa michezo mingi kwenye vilabu vyao?
Nmekuletea hizi takwimu za wachezaji wa ligi kubwa 5 barani ulaya kwa idadi ya majeraha waliyoyapata, siku walizokaa mpaka kupona hayo majeraha yote na michezo pia ambayo wameikosa.

1. Premier league( EPL)

Kwa upande wa ligi kuu kijana mwenye kipaji kikubwa raia wa uingereza na klabu ya arsenal Jack wilshere ndio anaongoza kwenye ligi hii akiwa amepata majeraha mara 13 akiwa ametumia siku 1013 kuuguza majeraha hayo yote .Jack wilshere amekosa michezo 155 mpaka sasa kipindi chote alichoapata majeraha hayo.

2.La liga (santander)

Kwenye ligi hii Thomas vermalein mchezaji wa fc barcelona pamoja na taifa ya ubelgiji ndio anaeongoza kwa majeraha mengi kwenye ligi hii akiwa ameumia mara 23 akiwa ametumia siku 1026 katika kuuguza majeraha yote ambayo ameyapata akiwa amekosa michezo 128 katika kipind chote cha majeraha.

3.Bundersliga

Kwenye ligi kuu ujerumani marco reus wa klabu ya dortmund na taifa la ujerumani ndio anaongoza kwa majeraha mengi zaidi akiwa ameumia mara 41 akiwa ametumia siku 813 kuuguza yote hayo ,huku akiwa amekosa michezo 104 akiwa katika kipindi hicho kigumu.

4.Seria A

Giuseppe rossi raia wa italy na klabu ya genoa ndio anaongoza kwenye ligi hii akiwa ameumia mara 7 akitumia siku 1194 kuuguza mjeraha hayo huku akiwa amekosa michezo 148 katika kipindi hicho chote.

5.Ligue 1

Katika ligi kuu nchini ufaransa mchezaji wa marseille na taifa la ufaransa Abou diaby ndio anaongoza akiwa ameumia mara 21 akitumia siku 2072 kuuguza majeraha hayo yote akiwa amekosa mechi 368 katika kipindi chote cha maisha yake ya soka.
Pengine ndio akawa mchezaji wa kwanza mwenye majeraha hatari ya soka kwenye ligi hizi


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz