KOCHA MWINYI ZAHERA ADONDOSHA WINO YANGA - EDUSPORTSTZ

Latest

KOCHA MWINYI ZAHERA ADONDOSHA WINO YANGA

Mwinyi Zahera
Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga. Hata hivyo, bado kuna hali ya sintofahamu.

Hali hiyo inatokana na ile kauli ya Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa kusema kwamba bado wanamuangalia Zahera na hawajampa mkataba.

Lakini baadaye kumekuwa na picha inazunguka mitandaoni na taarifa zinaeleza, Mkongo huyo amesaini miaka miwili.

"Sasa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC, kweli anaweza akaangaliwa Yanga. Jamani hata nyie angalieni hapo, amesaini mkataba tayari labda kuwe na jambo jingine au kocha kaona amekosea, kaamua kuondoka," kilieleza moja ya chanzo.

Zahera amechukua rasmi mikoba ya Mzambia aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco United.

Zahera alichelewa kusaini mkataba na Yanga kutokana na majadiliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo, lakini sasa wamefikia mwafaka na ameamua kuweka kandarasi hiyo itakayomalizika mwaka 2020.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz