SERIKALI KUANDAA MAANDAMANO YA MICHEZO APRIL 26 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Thursday, 5 April 2018

SERIKALI KUANDAA MAANDAMANO YA MICHEZO APRIL 26
Halmashauri ya jiji la Arusha imeandaa maandamano makubwa ya michezo ambayo yatafanyika siku ya sherehe ya maadhimisho muungano April 26, 2018 jijini Arusha

Afisa michezo wa jiji la Arusha, Benson Maneno amethibitisha hilo na kusema kuwa maandamano hayo yatafanyika asubuhi kuelekea katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume ambapo ndipo zitafanyika fainali za michuano ya Muungano Cup na kumpata mshindi wa michuano hiyo, ambapo mshindi wa kwanza atapata milioni mbili, mshindi wa pili milioni moja na mshindi wa tatu laki tano.

"Mashindano hayo ambayo yameanzishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa jiji la Arusha akishilikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Dakalo wameanzisha mashindano haya maalum kwa kata zote 25 ambapo watashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 26, hivyo kila kata itacheza na kata nyingine ili kupata mshindi wa michuano hiyo. Fainali hizo zitafanyika jioni lakini asubuhi ya tarehe 26 kutakuwa na maandamano makubwa ya wana michezo kuelekea uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume kwa ajili ya kufanya fainali hiyo ya Muungano CUP" alisema Benson Maneno.

Nini maoni yako!!!?  Tuachie ujumbe hapa chini 👇 Usikose kusubscribe

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.