-->

Type something and hit enter

OnImage result for yanga vs simba
kuelekea mechi ya leo kati ya watani wa jadi nchini tanzania Kocha wa Mwadui FC, Ally Bizimungu ametupia kura yake ya ushindi kwa simba sc na kusema Simba inaweza kushinda mchezo wa leo, Jumapili dhidi ya Yanga kama itawadharau wapinzani wao basi itakula kwao.

 Simba vinara wa Ligi Kuu wakiwa wamekusanya pointi 59 katika mechi 25 walizocheza, huku Yanga wakiwa nafasi ya pili kwa alama 48 kwa michezo 23 walizocheza. Bizimungu alisema kuwa kutokana na rekodi waliyoiweka Simba kwa msimu huu kucheza mechi 25 bila kufungwa ni sababu inayoweza kuwabeba katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Yanga. 

Alisema kuwa licha ya ubora wao kikosini, lakini wanapaswa kuwa na tahadhari kwani mpira hautabiriki haraka kutokana na presha za pande zote, hivyo wasidharau chochote hadi dakika 90 zimalizike. “Simba naona wamekuwa na mwendelezo mzuri kwenye Ligi Kuu, kwa sababu kucheza mechi 25 bila kupoteza si jambo dogo, ila niwashauri kutowadharau wapinzani wao,”alisema Bizimungu. 

Alisema kuwa nguvu, maarifa na mbinu walizotumia katika mechi zilizopita, ziwe zilezile watakazotumia dhidi ya mahasimu wao ili kuweza kufikia malengo yao. Aliongeza kuwa wanapaswa kuwa makini kutoruhusu mashambulizi ya aina yoyote na kutomtegemea mchezaji mmoja, badala yake kila mmoja apambane kuiokoa timu. “Wasiruhusu mashambulizi yoyote langoni mwao, kila mmoja apambane kuiokoa timu, wasimtegemee mchezaji mmoja kusaka ushindi,” alisema Kocha huyo.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Click to comment
 
Blog Meets Brand