USHINDI WA MAN U DHIDI YA LIVERPOOL WAMBAKIZA MANARA CCM - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

Saturday, 10 March 2018

USHINDI WA MAN U DHIDI YA LIVERPOOL WAMBAKIZA MANARA CCM


Kufuatia klabu ya Manchester United kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2 – 1 dhidi ya Liverpool, afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara kusalia katika chama chake cha Mapinduzi (CCM).

Mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliochezwa katika dimba la Old Trafford. ushindi unamfanya Manara kubaki, hii ni kutokana na ahadi yake aliyo itoa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa endapo timu yake hiyo pendwa ya United ingefungwa na Liverpool basi angekihama chama hicho na kujiunga na chama cha Chauma kinachoongoza na Hashim Rungwe.Aidha United imezidi kuwa mbabe kwa Liverpool licha ya kutawala kwa asilimia kubwa katika dakika zote 90, Liverpool ilifanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Eric Bailly kujifunga ikiwa ni dakika ya 66, baada ya kushindwa kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Sadio Mane.
baada ya kuitandika mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford leo, mechi ya Ligi Kuu England.

United imepata mabao yake kupitia Marcus Rashford, aliyefunga katika dakika ya 14 na 24 kipindi cha kwanza ambapo hadi dakika 45 za awali zinamalizika, United ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Hivyo United sasa imeendelea kusalia nafasi ya pili ikiwa na alama 65 dhidi ya Liverpool yenye 60.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ