TETESI ZA SOKA LEO TAREHE 10.03.2018 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Saturday, 10 March 2018

TETESI ZA SOKA LEO TAREHE 10.03.2018

Neymar mchezaji aliyesajiriwa kwa pesa nyingi kutoka Barcelona kwenda Psg

Mshambuliaji wa klabu ya Psg ya Ufaransa Mbrazil Neymar anajutia kuondoka katika klabu ya Barcelona na taarifa zinasema anataka kurejea klabuni hapo mwaka 2019 . (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester City wako tayari kuingia katika mbio za kumsajili kiungo Thomas Lemar mwenye umri wa miaka 22 kutoka klabu ya Monaco ya Ufaransa.(Telegraph)

Klabu ya Manchester United iko katika mawindo ya kutaka kumsajili mlinzi wa Fc Barcelona Samuel Umtiti's ambaye dau lake la kuuzwa ni pauni milioni 54.(Talksport)

Pia United wanataka kumsajili beki Sokratis Papastathopoulos, anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund na wamekuwa wakimfuatilia kwa ukaribu wiki hizi za karibuni . (Mirror)

Kiungo wa Chelsea Na Timu ya taifa ya Ufaransa Ngolo Kante amesema anavutiwa kidogo sana na kutaka kujiunga na miaka ya soka la Ufaransa .

Klabu ya Paris St-Germain licha ya timu hiyo kumfanya Ngolo Kante kuwa ndio mchezaji anayatakiwa kusajilia zaidi katika dirisha kubwa la usajili (London Evening Standard)
Bayern Munich

Beki kisiki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, anakaribia kujiunga na Juventus ya nchini Italia. (Bleacher Report, via Mirror)

Mshambuliaji wa Bayern Munich,Robert Lewandowski yuko huru kuweza kujiunga na Real Madrid hata hivyo Chelsea pia wako mstari wa mbele kuhakikisha wanaoata saini ya mchezaji huyo raia wa Poland. (Bleacher Report)

Meneja wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate yuko tayari kumpata mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane kitambaa cha unahodha wa timu ya taifa katika michuano ijayo ya Kombe la dunia(Star)West Ham inamuwania Okay Yokuslu.

West Ham inamuwinda kiungo wa Klabu ya Trabzonspor,Okay Yokuslu. Mwenye umri wa Miaka 23 kiungo huyu pia anawaniwa na Sevilla ya Hispania (AS - in Spanish)

Timu ya West Brom pia wanamfutilia mchezaji Okay Yokuslu, ambae ameichezea timu ya taifa ya Uturuki Mara tano (Milliyet - in Turkish)

Paris St-Germain Inataka kumarisha Safu yake ya ulinzi haswa upande wa kushoto kwa kutaka kuwasajili kinda wa Kingereza Ryan Sessegnon, mwenye miaka 17, Pamoja na Mbrazil Alex Sandro kutoka Juventus(Talksport)

Brighton wameungana na Crystal Palace na West Ham katika mbio za kumuwania kiungo wa Lille ya Ufaransa Ibrahim Amadou, 24. (Le10 Sport, via Sun)
Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 26 amesema hajakaribia kusaini mkataba mpya huku mkataba wake wa sasa unafikia mwisho ndani ya muda wa miezi mitatu ijayo. (Independent)

Mshambuliaji wa Everton Sandro Ramires ambae anachezea klabu ya Sevilla kwa Mkopo amesema anataka kusalia Sevilla kwa mkataba wa kudumu, Sandro alipelekwa klabuni hapo kwa mkopo mwezi januari. (Liverpool Echo)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ