USILOLIJUA KUHUSU EMMANUELI OKWI - EDUSPORTSTZ

Latest

USILOLIJUA KUHUSU EMMANUELI OKWI

Image result for EMMANUEL OKWI
Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea Jana kwa Simba kucheza na Mbao FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam
, wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Mwadui FCkatika uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga.
Baada ya Simba kupoteza point mbili Shinyanga kwa kutoka sare dhidi ya Mwadui FC, leo walionekana kufuta makosa na kuifunga Mbao FC magoli 5-0, magoli ya Simbayakofunhwa ma Shiza Kichuya dakika ya 38, Okwi aliyefunga mawili dakika ya 41 kwa penati na 68, Erasto Nyoni dakika ya 82 na Nikolaos Gyan dakika ya 86.
Game imemalizika kwa Okwi kuweka rekodi baada ya kufunga magoli mawili leo na kufikisha jumla ya magoli 16 akicheza game 15 VPL msimu huu, akivunja rekodi ya Abdurahman Musa wa Ruvu Shooting na Simon Msuva waliobuka wafungaji bora msimu uliyopita kwa kufunga jumla ya magoli 14 kila mmoja, hivyo Okwi kavunja rekodi hiyo akicheza game chache.
Ushindi huo sasa unaifanya Simba kufikisha jumla ya point 45 na kuendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Yanga waliyopo nafasi kwa kuwa na point 37 wakizidiwa mchezo mmoja.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz