UCHAMBUZI KUELEKEA MECHI YA PSG NA REAL MADRID - EDUSPORTSTZ

Latest

UCHAMBUZI KUELEKEA MECHI YA PSG NA REAL MADRID
Leo ni vita ya pesa kati ya matajiri wawili Real Madrid watakaowakaribisha Paris Saint German huku rekodi ya michezo yao iliyopita ikionesha kwamba kila timu imeshinda mara mbili nanpia wametoka suluhu mbili.

Msimu huu kati ya malengo makubwa ya matajiri wa Paris Saint German ni kubeba Champions League lakini katika mashindano matano ya Champions League yaliyopita PSG hawajawahi kupita kwenda robo fainali.

Lakini wakati PSG wakihangaika kuitafuta robo fainali, hali kwa wenzao Real Madrid ni tofauti kabisa kwani mabingwa hao watetezi katika mashindano saba yaliyopita ya Champions League wamefanikiwa kufudhu kwenda nusu fainali.

Santiago Bernabeu sio salama kabisa kwa mpinzani yeyote anayekanyaga kwani katika michezo 10/14 iliyopita Real Madrid walipata ushindi chini ya Zinedine Zidane na michezo yote 6 katika uwanja wa Santiago Bernabeu waliibuka kidedea.

Katika hatua kama hii ya mtoano PSG wamepoteza michezo minne kati ya sita ambayo wamecheza ugenini lakini msimu huu rekodi yao ya ufungaji inaogopesha sana kwani wameshaweka kambani mabao 25 katika hatua ya magrupu.

Kwa Gareth Bale huu unaweza kuwa mchezo wake muhimu kabisa kwani kama atakuwepo uwanjani hii leo baasi atakuwa amefikisha michezo 50 ya Champions League na kufikia rekodi ya Ryan Giggs kuwa mchezaji wa Wales wa pili kufikia idadi hiyo ya michezo.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz