KWA REKODI HII LIVERPOOL ATAKAMATIAKA DHIDI YA FC PORTO LEO? - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 14 February 2018

KWA REKODI HII LIVERPOOL ATAKAMATIAKA DHIDI YA FC PORTO LEO?

Liverpool wameshakutana na Fc Porto mara nne katika michuano tofauti lakini katika mara zote hizo Fc Porto hawajawahi kuwafunga Liverpool hata mara moja na kama wakifanya hivyo hii leo baasi itakuwa mara yao ya kwanza.

Hii ni mara ya kwanza kwa Fc Porto kufudhu kwenda katika hatua ya mtoano mara mbili mfululizo tangu wafanye hivyo msimu wa 2009/2010 lakini hawajawahi kwenda robo fainali tangu ule msimu wa 2004 ambao walibeba kombe.

Liverpool wanakwenda katika mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri sana kwani ni kati ya timu nne ambazo hadi hivi sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika Champions League msimu huu, timu nyingine ni Barcelona, Tottenham na Besiktas.

Hatari kubwa kwa Liverpool hii leo inaweza kuwa uwezo mkubwa wa Porto kupiga mipira ya “set-piece” ambapo katika msimu huu wa ligi ndio klabu ambayo inaongoza kwa ufungaji wa mabao ya “set-piece” (mabao 8).

Uwanja wa klabu ya PSG “Parc Des Princes Stadiym” ndio uwanja unaoongoza kwa kuzalisha mabao mengi katika CL msimu huu(16) lakini unaofuatia ni uwanja wa Fc Porto “Portos Dragao” (mabao 15).
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ

No comments:

Post a Comment