SOMA ALICHOCHANGIA NAPE MNAUYE BUNGENI KUHUSUIDARA YA USALAMA WA TAIFA - EDUSPORTSTZ

Latest

SOMA ALICHOCHANGIA NAPE MNAUYE BUNGENI KUHUSUIDARA YA USALAMA WA TAIFA


Image result for NAPE MNAUYE
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu
wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania.

Nnape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali, kukumbuka jukumu lao la la kuhakikisha wanalinda uchumi nchi katika kipindi hichi, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine.

Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amemjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa sio kutafuta watu waliopotea au kuumizwa kama wanavyodai na laiti wangelifahamu wanachokifanya wangekaa kimya.

"Kazi ya usalama wa Taifa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi tu mimi nasema hoja mlizozitoa kuhusu idara kwamba haishauri serikali mambo ya uchumi na mambo mengine hamna ushahidi", amesema Kapteni Mkuchika.

Pamoja na hayo, Kapteni Mkuchika ameendelea kwa kusema "sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, kazi zilizopitishwa kwa mujibu wa Bunge kuna shughuli nne za idara kwamba ni kukusanya na kutafuta habari pamoja na kuzifanyia tathmini na wanapoyafanya hayo hawayafanyi katika mkutano wa hadhra, kushirikiana na vyombo vya idara nyingine vinashughulikana na usalama wa nchi, kuwashauri Mawaziri ili waishauri serikali na mambo yote ya kuujumu uchumi na vingine wanayafanya kimya kimya".

Kwa upande mwingine, shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taifa zimehairishwa jana jioni (Ijumaa) mpaka Aprili 03 mwaka 2018.
Elimu Yetu
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz