SABABU ZA CHIRWA KUTOKWENDA SHELISHELI ZAGUNDULIKA - EDUSPORTSTZ

Latest

SABABU ZA CHIRWA KUTOKWENDA SHELISHELI ZAGUNDULIKA

Image result for obrey chirwa yanga
Straika nyota wa Simba, Emmanuel Okwi, ameonekana kumuumiza kichwa straika wa Yanga, Obrey Chirwa ambapo imebainika kuwa ndiye chanzo cha Mzambia huyo kushindwa kuungana na wenzake kwenye safari ya kuelekea Shelisheli kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Louis.


Chirwa alishindwa kuungana na wenzake wa Yanga walioelekea nchini Shelisheli kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya St Louis, baada ya kupata majeraha ya misuli ya nyama za paja, jambo ambalo lilisababisha kubakizwa jijini Dar.


Taarifa kutoka ndani ya Yanga kimeeleza Okwi ndiye aliyechangia Chirwa ashindwe kwenda Shelisheli baada ya kulazimisha kucheza mchezo wao wa ligi kuu uliopita dhidi ya Majimaji huku akiwa na majeraha ambapo alipanga kuongeza idadi ya mabao ili kumpita Mganda huyo.


“Ukweli ni kwamba Okwi ndiye ambaye amechangia Chirwa kubakia hapa Dar baada ya kushindwa kwenda Shelisheli kama wenzake ambavyo walifanya kwa sababu Chirwa alilazimisha kucheza ile mechi na Majimaji huku akiwa anaumwa.


“Yeye alipanga atumie mchezo ule kama sehemu ya kumzidi Okwi mabao sasa bahati mbaya ni kwamba baada ya mchezo kumalizika lile jeraha likazidi kuwa kubwa hivyo kusababisha hadi jina lake litolewe katika wale ambao wanasafiri kuelekea nchini humo kwa ajili ya mchezo wetu.


“Hata hivyo, sasa hivi bado anatamani kupona haraka kwa kuwa anataka kurudi uwanjani mapema ili afunge na awe mfungaji bora wa ligi,” kilisema chanzo hicho.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz