MAGONJWA UNAYOTAKIWA KUYAPIMA NA KUYAJUA KABLA YA KUFUNGA NDOA - EDUSPORTSTZ

Latest

MAGONJWA UNAYOTAKIWA KUYAPIMA NA KUYAJUA KABLA YA KUFUNGA NDOA



NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

1. Ugonjwa wa kaswende.Kitaalamu kama syphilis, huu ni ugonjwa hatari sana ambao umeharibu maisha ya watu wengi bila wao kujifahamu. Ugonjwa huu ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiana huanza kidogo na kidonda ambacho hakiumi sehemu ambapo wadudu wamepita mfano mdomoni au sehemu za siri.

Kidonda hicho hupona, upele usiowasha hutokea na baadae vyote hivyo hupotea. Ugonjwa huu baadae huingia ndani ya mwili na kuuanza kuharibu viungo vya ndani. Mwisho kabisa ugonjwa huu huahamia kwenye ubongo na kumfanya mtu kua kichaa.

2. Ugonjwa wa hepatitis B.Ugonjwa huu ni hatari na unaua haraka kuliko ukimwi, virusi vya ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiana na kugusana kwa damu au majimaji ya mwili kama ukimwi lakini ni rahisi zaidi kuambukizwa ugonjwa huu kuliko kupata ukimwi.

Ugonjwa huu hushambulia maini na kuacha makovu, Mgonjwa hupata macho ya njano, homa, maumivu ya kichwa na kadhalika. Ugonjwa hii mwishoni hupelekea kansa ya ini ambayo inaua ndani ya miezi sita.

3. Ugonjwa wa ukimwi.Huu ni ugonjwa unaofahamika kwani unatangazwa sana hasa kwenye vituo vya Radio, Tv, Magazeti na sehemu mbalimbali.

Ugonjwa huu uligundulika karne ya 20 na mpaka sasa umeshaua watu wengi sana na zaidi ya 95% ya wagonjwa waliambukizwa kwa kushiriki ngono bila kinga.

4. Ugonjwa wa gonorea.Huu ni ugonjwa wa zinaa ambao unashambulia jinsia zote yaani Wanaume na Wanawake, mara nyingi Mwanaume hawezi kujificha na ugonjwa huu kwani dalili za ugonjwa huo kama kutoka na usaa kwenye njia ya kukojolea zitamuumbua lakini kwa wananwake ugonjwa huu huweza kukaa kimya na mwana mke hujikuta akisambaza ugonjwa huo bila kujua. Mwishoni ugonjwa huu hushambulia kizazi na kusababisha ugumba. EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz