KIMEWAKA, TAZAMA ALICHO KIPOSTI MANEGER WA DIAMOND KUHUSU RUGE WA CLOUDS - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Thursday, 8 February 2018

KIMEWAKA, TAZAMA ALICHO KIPOSTI MANEGER WA DIAMOND KUHUSU RUGE WA CLOUDS


Image result for MANAGER WA DIAMOND
Meneja wa label ya WCB, Sallam SK amefunguka kwa kuendelea kudai kw Fmamba kampuni yao haina tatizo na chombo chochote cha habari isipokuwa Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na Clouds TV ndio mwenye tatizo na label hiyo.

Mapema wiki hii meneja huyo alianza kwa kuandika ujumbe mtandaoni unaodai kuna mtu anataka kumshusha Diamond huku akidai hakuna mtu wa kumshusha katika utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.
Sallam ameendeleza mashambulizi hayo ambapo jana amemtaja mtu aliyedai kwamba ana njama za kumshusha Diamond.


“Kwa heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKaa,” aliandika Sallam kupitia Instagram.


Meneja huyo anaonekana kutaka kuendeleza harakati hizo kwani toka aanze kutoa waraka huo amekuwa akiweka hushtag ambayo imekuwa ikitumika na Clouds Media, #TumekataaKuwaKaa.


Ruge bado hajazungumza chochote kuhusiana na tukio hili


Elimu Yetu

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mnoEdusportstz↑ Grab this Headline Animator

No comments:

Post a Comment