HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA SIMBA KUHUSU AISHI MANULA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 20 February 2018

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA SIMBA KUHUSU AISHI MANULA

Image result for aishi manula
Uongozi wa Simba umesema kipa wake Aishi Manula anaendelea vizuri na kuna asilimia 90 za yeye kucheza mechi ya kesho dhidi ya Gendamarie.

Simba iko nchini Djibouti tayari kuivaa Gendamarie katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho. Simba ilishinda kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza jijini Dar.


Benchi la ufundi limeeleza kwamba kinachomsumbua Manula baada ya kuupia leo ni kidole.


“Daktari amesema hadi asubuhi atakuwa na la kusema ingawa anaona kwa asilimia tisini ana nafasi ya kucheza. Kama hakitakuwa kimevimba asubuhi, basi atakuwa tayari kucheza kama akipangwa na mwalimu.


“Tayari alianza kupatiwa huduma pale uwanjani na baadaye usiku huu na tunaamini ataamka vizuri,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ