AZAM USO KWA USO NA KMC KESHO

Image result for azam
Hatua ya mzunguko wa Nne (4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inaendelea
Jumamosi Februari 24, 2018 kwa michezo miwili.
Singida United watakuwa Uwanja wa Namfua Mjini Singida kucheza na Polisi Tanzania saa 10 jioni na mchezo mwingine utakaohitimisha siku hiyo utakuwa kati ya KMC watakaokuwa nyumbani Azam Complex, Chamazi kuwakaribisha Azam FC saa 1 usiku.
Mzunguko huo wa Nne (4) utaendelea tena Jumapili Februari 25, 2018 kwa Buseresere kuwaalika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam mchezo ukichezwa saa 10 jioni nao Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania Azam Complex Chamazi saa 1 usiku.

Mzunguko huwa wa 4 utakamilika Jumatatu Februari 26, 2018 Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.
Enter your email address:


Delivered by EDUSPORTSTZ
Subscribe to EDUSPORTSTZ

Artikel Terkait