ZIJUE ZINAZOKIKI KATIKA TETESI ZA SOKA ULAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

ZIJUE ZINAZOKIKI KATIKA TETESI ZA SOKA ULAYA


Eden Hazard

Real Madrid wanajiandaa kutoa ofa ya pauni milioni 120 kwa mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Sun)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekana kuwepo tofauti kati ya mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, na wachezaji wengine. (Sky Sports)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, amekataa kukana kuwepo jitihada mpya kwa Sanchez baada ya Gabriel Jesus kupata jeraha wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili. (Talksport)Theo Walcott

Southampton wanataka kumsaini wing'a wa Arsenal Theo Walcott 28, kwa mkono Januari hii. (Mail)

Na Arsenal wanaweza kumuchia mchezaji huyo kuondoka huku Everton, Watford na West Ham wakiwa na dalili za kumsaini. (Mirror)

Manchester United wanatumai kuwa kiungo wa kati Paul Pogba anaweza kumsaini mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala, 24, kujiunga na klabu hiyo.Joao Mario

Naye meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kiungo wa kati wa Inter Milan Joao Mario 24, kuchukua mahala pake Michael Carrick, 36. (Sun)

Tottenham hawako mbioni kuafikia mkataba mpya na mlinzi Toby Alderweireld, 28, licha ya mkataka wake wa sasa kumruhusu kuondoka msimu wa joto wa mwaka 2019 kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka, 22, atajiunga na Bayern Munich msimu huu. (Bild - in German)EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz