TETESI ZA SOKA LA ULAYA IJUMAA YA LEO TAREHE 12.1.2018 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 12 January 2018

TETESI ZA SOKA LA ULAYA IJUMAA YA LEO TAREHE 12.1.2018


Image captionArsene Wenger na Alexis Sanchez

Manchester United imewasilisha ombi la dau la £25m kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na raia wa Chile Alexis Sanchez. (Guardian)

Sanchez angependelea kujiunga na Manchester City, lakini kikosi cha Pep Guardiola kinataka kumsajili mchezaji huyo kwa £20m pekee. (Independent)

Manchester United pia wanawataka washambuliji wawili akiwemo mshambuiaji wa Leicester na Uingereza ,30, Jamie Vardy na mwenzake wa West Ham, 29, Javier Hernandez, ambaye alikuwa katika uwanja wa Old Trafford kutoka 2010-2015. (Telegraph)

Klabu ya ligi ya New MLS nchini Marekani Los Angeles FC pia inamtaka Hernandez. (Talksport)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte huenda akaondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mkufunzi wa Juventus Massimiliano Allegri na aliyekuwa kocha wa Barcelona Luis Enrique wanaongoza kurithi mahala pake. (Mail)

Manchester United na Chelsea wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo, 21, kutoka Gremio. (Star)

Liverpool wameanza mazungumzo na Leicester na winga wa Algeria Riyad Mahrez, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anataka kujiunga na Arsenal (Express)

Liverpool inawasiliana na klabu ya RB Leipzig huku wakijaribu kumchukua mshambuliaji Naby Keïta kama mrithi wa Philippe Coutinho's aliyehamia Barcelona.

Mpango tayari umeafikiwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kujiunga na klabu hiyo mwezi Julai.(Times)

Liverpool iko tayari kumuuza mshambuliaji wao mwenye umri wa miaka 28 Daniel Sturridge, lakini watahitaji £30m ili kumuuza mshambuliaji huyo wa Uingereza. (Liverpool Echo)

Hatahivyo hakuna klabu katika ligi ya Uingereza ilio na uwezo wa kumunua mchezaji huyo mbali na mshahara wake wa £150,000 kwa wiki . (Mail)

Italian Carlo Ancelotti ndiye kocha anayepigiwa upato kumrithi mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger mwishoni mwa msimu huu .

Kocha huyo wa zamani aliyewahi kuifunza Chelsea, Real madrid, Bayern Munich na Paris St Germain amekubali mkataba wa miaka minne wenye thamani ya £35.5m. (Corriere dello Sport - in

Everton inajiandaa kuwasilisha ombi la £20m ili kumsajili winga na mshambulijia wa Arsenal Theo Walcott. (Telegraph)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ