SANCHEZ KUJIUNGA NA MAN U MKHITARYAN NAYE AKUBALI KWENDA ARSENAL - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 21 January 2018

SANCHEZ KUJIUNGA NA MAN U MKHITARYAN NAYE AKUBALI KWENDA ARSENAL


NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
Mkhitaryan alijiunga na Manchester United kutoka Borussia Dortmund miaka miwili iliyopita

Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya Manchester United Henrikh Mkhitaryan amekubali kujiunga na timu ya Arsenal, huku Alexis Sanchez akitarajiwa kuhama upande wa pili.

Mkhitaryan, mwenye umri wa miaka 28,ambaye ni raia wa Armeniaatafanyia ukaguzi wa kimatibabu Leo Jumapili au kesho Jumatatu, huku Sanchez mwenye umri wa miaka 29 raia wa Chile atafanyiwa ukaguzi leo Juampili.

Muda wa mkataba wa Mkhitaryan na kitita atakachopokea kama mashahara hakijulikani.

Arsene Wenger awali alisema Sanchez atajiunga na United iwapo tu Mkhitaryan atahamia Arsenal.

Sanchez alikosa ushindi wa Arsenal wa mabao 4-1 dhidi ya Crystal Palace Jumamosi kwasababu alikuwa anasafiri kwenda Manchester.

"Huwezi kusafiri kwenda kaskazini na ucheze soka kwa wakati mmoja," alisema Wenger.Alexis Sanchez

Mkufunzi wa United Jose Mourinho, wakatihuo huo amesema mkataba wa kumsajili Sanchez unakaribia kukamilika kufuatia ushindi wa timu yake wa bao 1-0 dhidi Burnley Jumamosi.

Timu hiyo ya Mashetano wekundu iliipiku Arsenal kumsajili Mkhitaryan kutoka Borussia Dortmund mnamo July 2016 kwa kima cha £ milioni 26.3.

Sanchez, amefunga mabao 80 katika mechi 166 za mashindano yote akiichezea Arsenal tangu kusajiliwa kutoka Barcelona mnamo July 2014 kwa £ milioni 35.

Raia huyo wa Chile ambaye mkataba wake na Arsenal ulitarajiwa kumalizika msimu wa joto mwaka huu alitarajiwa kusajiliwa Manchester City mwaka jana.

Imeabinika wiki hii kwamba City iliamua kutomsajili tena.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ